SAFARI YA MWISHO YA MSANII ALBERT MANGWEHA YATIKISA DAR NA MOROGORO LEO
Maelfu
ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake leo wameshiriki
kuaga mwili wa msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Albert
Kenneth Mangweha 'Ngwair' aliyefariki dunia ghafla Mei 28 mwaka huu huko
nchini Afrika Kusini. Mwili wa marehemu Mangweha kwa sasa tayari
umewasili mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayofanyika kesho huku
maelfu ya wananchi wa Morogoro wakiwa wametanda barabara kuaga
mwili huo
Ilikuwa ni simanzi kwawale hasa
waliokuwa wakipata Burudani kutoka kwa Albert Mangwair na hakika
aliyethibitisha kwa kuona kuwa sasa amelala na hainuki hadi Masiha
atakapo rudi walishindwa kujizuia kwa vilio kama Rasta huyu kutoka
Ukonga Mazizini maarufu kwajina la Simaga akitokwa na machozi baada ya
kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Albert Mangwea katika
viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mamia ya Wakazi wa jiji
walijitokeza kumuaga Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya aliyefariki
Mei 28, mwaka huu Nchini Afrika Kusini alikokuwa kwa shughuli za
kimuziki.
Mangwewa alisafirishwa mchana wa leo kwenda Kihonda mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayo fanyika kesho.
Wasanii wa Bongo Movie wakipita kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa marehemu.
Wasananii wa muziki nao wakipita kutoa heshima za mwisho.
Hata wanahabari nao kama Issa Mnali walitoa heshima za mwisho.
Ras Simaga akipita na zana zake baada ya kutoa heshima za mwisho.
Miraji Kikwete akizungumza machache na Ummy Wenselaus 'Dokii' viwanja vya Lidaz
Juu ni wana Dar es Salaam wakiwa katika folenina chini watu wachache waliokuwa wameketi.
Wanafamilia wakiwa katika jukwaa lao.
Wadau wakubwa wa kazi za Ngwair wakiwa katika pozi la majonzi.
Wakazi
wa jiji wakiwa na majonzi lakini FK Blog imebaini kuwa misiba ya
wasanii hujaa watu wengi lakini si wote wanaenda kuomboleza bali wengine
hufika kwaajili ya kuwaona 'LIVE' wasanii tofauti na walivyozoea katika
luninga.
Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya Ngwair ikiwa jukwaani.(PICHA NA http://mrokim.blogspot.com
Reviewed by crispaseve
on
10:11
Rating:
Post a Comment