TBL YASHINDA TUZO YA MAZINGIRA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick akimkabidhi tuzo Ofisa
Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu baada ya kampuni
hiyo kuibuka mshindi wa kwanza kwa kusaidia utunzaji wa
mazingira,katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani,
yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Zakheim, Mbagala, Dar es Salaam
leo. Wanaoshuhudia ni Ofisa wa Afya na Usalama Kazini wa TBL, Ismail
Kalema (wa pili kulia) na Meya wa Temeke wa Manispaa ya Temeke, Maabad
Hoja.
Mratibu wa Afya na Usalama Kazini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Daud Lwila (katikati), akionesha tuzo ya cheti baada ya kukabidhiwa na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick kwa kuwa kampuni ya kwanza
kusaidia utunzaji wa mazingira katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya
Mazingira Duniani,yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Zakheim,
Mbagala, Dar es Salaam
Wafanyakazi wa TBL, wakiwa na tuzo hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick akiwa katika picha ya pamoja
na taasisi zilizozopewa tuzo Mazingira. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa
TBL, Doris Malulu.
Doris Malulu na ImailKalema wa TBL wakiwa pamoja na wananchi walishiriki kwenye maadhimisho hayo.
Wasanii wa Bendi ya Mjomba, wakitumbuiza kwa sarakasi wakati wa maadhimisho hayo.
Mjomba Band ikitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Reviewed by crispaseve
on
10:12
Rating:
Post a Comment