Header AD

TASWIRA YA TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2013.

 
Omy Dimpoz akiwa ameshikilia moja ya tuzo zake na Vanesa Madee .Kushoto ni Wema Sepetu ambaye alimkabidhi tuzo hiyo.
 Kala Jeremaya akionesha ishara ya Amani mara baada ya kupokea tuzo yake mojawapo katika ya tatu alizo pata.
 Mkurugenzi wa Montage Limited, Teddy Mapunda akiwa na Halidi Chokoraa mara baada ya Chokraa kuipokea tuzo ya Hadija Kopa ambaye amefiwa na mumewe hivi karibuni.
 Mwandaaji wa Muziki Man Walter a.k.a Man Maji akiwa ameshikilia tuzo yake ya Mwandaaji bora wa Mwaka wa Bongo Fleva.
 Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ kulia akiangalia Tuzo yake ambaye imeshikiliwa na Ditto aliyo itwaa kupitia wimbo wake wa Chocheeni Kuni.
 Thabit Abdul akizungumza mara baada ya kupokea tuzo yake ya Mtuzi bora wa Mashairi ya Taarab.
 Hapa ilikuwa tuzo iliyokwenda kwa Rama D ya wimbo bora wa R&B.
 Mfalme wa Rymes, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ akitumbuiza.
 Msanii wa midundo ya asili Saida Karoli akitoa burudani kwa wageni mbalimbali.
 wasanii kutoka kundio la Worrios wakionesha tuzo yao ya Wimbo Bora wa Rege waliyoipata kupitia Wimbo wa Kilimanjaro.

 Msanii wa Muziki wa Kizazi,Kala Jeremiar akitoa shukrani zake kwa mashabiki waliompigia kura na kumuwezesha kupata Tuzo tatu zikiwa ni Msanii Bora wa Hip Hop,Mtunzi Bora wa Mashairi ya Hip Hop pamoja na Wimbo Bora wa Hip Hop kwa kipindi chote cha Mwaka 2012/13.Kulia ni Msanii Shilole aliepanja jukwaani Kumsindikiza.Hafla hii ya utoaji tuzo imefanyika Usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.
 Msanii Mkongwe wa Muziki wa Hip Hop hapa nchini ambaye sasa amepotea kidogo kwenye Gemu hilo,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crezy G.K akiwasalimia mashabiki wake pindi alipopanda jukwaani kutoa tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop.
DJ Mseto toka Citizen TV ya Kenya akimuwakilisha mwanamuziki Jose Chamilione baada ya kupata tuzo ya Wimbo bora wa Afrika Mashariki.
Ommy Dimpoz kwa Pozi aliondoka na tuzo tatu usiku wa kuamkia leo pale Mlimani City,jijini Dar
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kushila Thomas (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na kiongozi wa Bendi ya The Kilimanjaro (wana njenje),Waziri Ally pamoja na Mwana FA baada ya kukabidhi tuzo ya heshima kwa bendi hiyo,wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki mbali mbali iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Konyagi,David Mgwassa (kushoto) akikabidhi tuzo ya heshima kwa 
Redd’s Miss Tanzania 2012,Brigit Alfred akikabidhi tuzo ya Msanii Bora wa Kike iliyokwenda kwa Bint Komando Lady Jay Dee.Anayeipokea tuzo hiyo ni Mumewe Lady Jay Dee,Ndugu Garder Habash.
G. Habash akizungumza kwa niaba ya Lady Jay Dee.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,George Kavishe akitangaza mshindi wa tuzo Msanii Bora wa Bongo Flava.
Muwakilishi wa Msanii Diamond akishukuru kwa niaba yake.
Mtunzi Bora wa Mashairi ya Muziki wa Taarab ni Thabit Abdul na hapa akipongezwa.
Khareed Chokoraa akichukua tuzo ya Msanii Bora wa Kike,ambayo ilikwenda wa Mkongwe Khadija Kopa.
Wawakilishi wa Isha Mashauzi wakipokea tuzo ya Msanii Bora wa Kike Taarabu kutoka kwa Mkurugenzi wa Aset,Baraka Msilwa.
Mrisho Mpoto na Ditto wakipokea tuzo ya Wimbo bora wenye vionjo vya asili.
Ben Pol akinyakua tuzo ya msanii bora wa kiume.
Ben Pol akishuru mashabiki pamoja na Mama yake.
Tuzo ya Prodyuza bora wa Mwaka ilienda kwa Man Water.
 Man Water akitoa shukrani.
Wema Sepetu akitangaza mshindi wa Tuzo ya Video Bora ya Mwaka iliyokwenda kwa Ommy Dimpoz.
Ommy Dimpoz na Vannesa Mdee wakipokea tuzo kutoka kwa Wema Sepetu.
//
Reviewed by crispaseve on 07:58 Rating: 5

No comments

Post AD