WAZIRI MKUU ATOA SH. MILIONI 10 KUSAIDIA VIJANA 87 WAJITEGEMEE
WAZIRI MKUU Mizengo
Pinda ameahidi kutoa sh. milioni 10 ili kuwasaidia vijana wanaoishi
kwenye kijiji cha vijana cha Tulu ambao wameamua kujitegemea kwa
uzalishaji kupitia kilimo, matumizi ya misitu na ufugaji.
Alitoa ahadi hiyo jana
jioni (Alhamisi, Agosti 29, 2013) wakati akizungumza katika mkutano wa
hadhara na vijana wa kijiji hicho pamoja na wakazi wa vijiji jirani vya
Tumbili na Lufwisi wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Kijiji cha Vijana cha
Tulu ambacho wenyewe wanakiita Pathfinders Green City (Jiji la Watafuta
Njia) kilianzishwa Aprili 2013 kikiwa ni msitu mtupu baada ya kupewa
ekari 280 kutoka vijiji jirani vya Tumbili na Lufwisi. Kilianzishwa
kikiwa na vijana 68 kutoka katika kata zote 17 za Wilaya ya Sikonge.
Hivi sasa kijiji kina vijana 87 wakiwamo wasichana 22 na wavulana 65
wenye umri wa kati ya miaka 18 na 24.
Reviewed by crispaseve
on
09:34
Rating:
Post a Comment