Exclusive: Ostaz Juma amrudisha Janjaro Watanashati baada kuahidi kubadilika, Janjaro asema 'yamekwisha'
Siku
moja baada ya Boss wa Watanashati Ostaz Juma na Musoma kutangaza kuwa
amemfukuza Janjaro kwenye kundi la watanashati kwa sababu za utovu wa
nidhamu, C.E.O huyo ameamua kumrudisha tena kundini rapper huyo.
Ostaz
Juma ameiambia tovuti ya Times fm exclusively kuwa ameamua kumrudisha
kundini Janjaro kwa kuwa ameonesha hali ya kuelewa na kumhakikishia
kwamba amebadilika .
“Nimeamua
kumrudisha, kwa sababu yale mambo yaliyopelekea mpaka mimi kutoa
maamuzi yale niliyotoa jana, yaani kawa kama mtu mzima mwenye akili
timamu, na mtu yeyote anayelifikiria na akaona kwamba hili ni kosa
akasema kwamba ntajirudi, ni kumpa nafasi ya kumsikiliza.
“Kwa
hiyo jana tulikaa kama kikao cha familia nyumbani kwangu, tukazungumza
na ni kweli ameona kwamba ni bora aache baadhi ya mambo ambayo hayakuwa
mazuri kwenye jamii, na mimi nachokitaka dogo Janja awe mtu bora, awe
mzuri katika jamii. Na yeye ameniahidi kwamba, atawahakikishia
watanzania kwamba atakuwa dogo janja ambae watanzania wanamtaka wao.”
Amesema Ostaz Juma.
Janjaro ameiambia tovuti hii kuwa bado yuko watanashati na kwamba ile tofauti kati yao ilimalizika baada ya kikao.
“
Mi niko mtanashati, kwa sababu ni mambo ya kifamilia na tumeshakuwa
familia moja, na mimi naona kuhamahama sio swala zuri, na kama nilikuwa
na malengo ya kufanya kazi nzuri, ni bora niendelee kupalilia tu
hapahapa. Yamekwisha isha kwa ufupi.”
Kuhusu wapi alikosea na anaona hatakiwi kurudia tena,janjaro amewatupia lawama 'marafiki' kwa kuwa chanzo cha yote.
“Kwa
namna moja ama nyingine ni ile chuki, marafiki ambao wamenizunguka, ni
watu ambao ni soo, sio watu wazuri. Sasa hivi rafiki yangu hela tu.”
Janjaro
na Ostaz Juma kwa pamoja wameahidi kuendelea kutoa burudani kwa fans
wao,ambapo Ostaz amesema sasa hivi amejipanga zaidi kama msanii na
ataachia ngoma nyingi kali akiwa na wasanii wengine wa kundi la
Watanashati.Chanzo Times Fm
Reviewed by crispaseve
on
01:42
Rating:
Post a Comment