Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi.
Rais Jakaya Kikwete
------
Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa
mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa
hailingani na utendaji wao wa kazi.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana jijini Dar es
Salaam, imeeleza kuwa viongozi hao wanalipwa mishahara inayotofautiana
kwa kiwango kikubwa na pato la mwananchi wa kawaida.
Huku ikitaja mapato ya mishahara ya marais wa
baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania, imesema kuwa hali
hiyo ni kuibebesha jamii mzigo wa kugharimia malipo ya viongozi.
Akizindua ripoti hiyo iliyochunguza gharama za
kuwalipa viongozi wa Serikali na wanasiasa, Mtafiti kutoka Taasisi ya
Utafiti kuhusu Kuondoa Umaskini (Repoa), Dk Theodore Valentine, alisema
kuwa viongozi wa Afrika Mashariki ndio wanaoongoza kwa kulipwa mishahara
mikubwa zaidi chini ya Jangwa la Sahara.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.......
Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi.
Reviewed by crispaseve
on
22:15
Rating:
Post a Comment