MAN UNITED NA ROONEY KUFUNGUA MAZUNGUMZO YA MKATABA MPYA WA PAUNI MILIONI 50, MOYES AHAHA KUIMARISHA KIKOSI

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
MANCHESTER
United wanaamini kuwa mshambuliaji wao Wayne Mark Rooney yuko tayari
kwa mazungunmzo ya mkataba mpya wa miaka minne utakaogharimu thamani ya
pauni milioni 50.
David
Moyes anajiandaa kuongeza nguvu katika kikosi chake katika dirisha dogo
la usajili (Januari mwakani) ili kuweza kuendana na kasi ya msimu huu
ambao Man United inasuasua sana.
Mwenyekiti
wa United Ed Woodward amewasiliana mara kadhaa na wakala wa Roney,
Bwana Paul Stretford na inafahamika kuwa kikao rasmi kitafanyika siku
chache zijazo.
Mambo Supa: Manchester United wanafanya mpango wa kufungua mazungumzo na mshambuliaji wao Wayne Rooney
Ni
mara ya kwanza kwa klabu kutoa taarifa hiyo tangu kuvunjika kwa
mahusiano mazuri baina ya kocha wa zamani wa Man United, Sir Alex
Ferguson na Rooney ambapo kibabu alisema nyota huyo, 28, aliomba
kuondoka, lakini mchezaji huyo mara zote anakataa maneno hayo.
Taarifa
za kubakia kwa Rooney zinampa raha Moyes ambaye anataka kuwatoa kafara
baadhi ya wachezaji na kusajili wapya ili kuimarisha kikosi chake.
Ashley
Young, Nani na Antonio Valencia bado wanajitahidi kutafuta njia ya
kubaki na Moyes amesema: ‘Wachache wanaweza kuondoka kama tutapata ofa
nzuri.’


Wachezaji
wawili wa England Tom Cleverley na Danny Welbeck, pia Javier Hernandez,
Anderson na Alex Buttner, hawajathibitisha kubaki au la, wakati
Mkongwe Rio Ferdinand na Patrice Evra inaonekana klabu haina mpango wa
kuwapa ofa ya mkataba mpya
“Nimejaribu kutoa nafasi kwa kila mtu; alisema Moyes. “Tutauza?, Kama tutapata ofa nzuri pengine tutaangalia hilo”.



”Tutajaribu kuweka usawa kwa kuondoa watu, lakini pia kuwaleta watu”. Alisema Moyes.
Moyes
anatupia ndoana zake kwa kiungo wa Atletico Madrid, Koke Face, kwa dau
la pauni milioni 15, pia beki wa Porto, Eliaquim Mangala aliowaona
kwenye michuano ya UEFA jumatano ya wiki hii. Pia anafanya mipango ya
kutuma tena ofa kwa beki wa kushoto wa Everton, Leighton Baines.
MAN UNITED NA ROONEY KUFUNGUA MAZUNGUMZO YA MKATABA MPYA WA PAUNI MILIONI 50, MOYES AHAHA KUIMARISHA KIKOSI
Reviewed by crispaseve
on
02:29
Rating:
Post a Comment