Shughuli ya Mazishi ya Mzee Nelson Mandela hivi sasa kijijini Qunu
Kamera
ya Globu ya Jamii ipo Ndani ya Hema maalumu ambamo shughuli ya mazishi
ya marehemu Nelson Mandela inaendelea hivi sasa katika kijijini Qunu.Na
kama ilivyo ada ya libeneke la Globu hili kwamba halilali na litakuwa
linakuletea Live matukio yote yanayoendelea katika Mazishi ya Shujaa
huyo wa Afrika na Dunia kwa Ujumla.
Rais Jakaya Kikwete akitoa historia fupi ya Marehemu Mzee Nelson Mandela kuhusiana na mahusiano aliyokuwa nayo na Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete akitoa historia fupi ya Marehemu Mzee Nelson Mandela kuhusiana na mahusiano aliyokuwa nayo na Tanzania.
Rais
Jakaya Kikwete ni mmoja wa viongozi mbalimbali wanaoshiriki kwenye
mazishi ya hayati Mzee Nelson Mandela yanayofanyika leo kijijini kwao
Qunu, nchini Afrika Kusini.
Watu
wengi maarufu Duniani wapo eneo hili hivi sasa kuhudhuria mazishi ya
Mzee Nelson Mandela yanayoendelea hivi sasa katika kijiji cha
Qunu,baadhi yao ni Oprah Wilfrey,Forest Whitaker,Richard Branson,Idris
Ebra na wengine wengi.
Mwili wa Mzee Mandela ukiwasili ukumbini.
Rais wa Zamani wa Zambia,Mzee Keneth Kaunda pia yupo.
Ankal
akisalimiana na Mcheza Filamu,Idris Elba ambaye amecheza Filamu ya Long
Walk to Freedon inayoelezea mapambano ya Mzee Mandela wakati alipokuwa
akihangaika kuutafuta uhuru wa mtu mweusi nchini Afrika kusini.
Shughuli ya Mazishi ya Mzee Nelson Mandela hivi sasa kijijini Qunu
Reviewed by crispaseve
on
02:34
Rating:
Post a Comment