WANAFUNZI WA UDAKTARI MUHIMBILI HATARINI
-AMA KWELI MGANGA HAJIGANGI
WANAFUNZI
wanaosomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (Muhas) wanaishi katika mazingira hatarishi kwani wanaweza
kupata magonjwa ya mlipuko na yale ya kuambukizwa wakati wowote.
Uchunguzi
uliofanywa na Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ndani
ya majengo ya chuo hicho yaliyo karibu na taasisi ya mifupa (MOI),
umegundua kwamba kwa miezi mingi, vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi hao
vimejaa na kuziba kabisa, hali inayowafanya vijana hao, licha ya
kushindwa kupata huduma hiyo muhimu ya kibinadamu, pia kuwa katika
hatari ya kupatwa na magonjwa ya mlipuko.
“Hali
ni mbaya sana hapa kwa kweli. Hatuna huduma ya choo kwa miezi miwili
hadi mitatu sasa, tunapobanwa na haja, hasa kubwa, hulazimika kukimbilia
Kariakoo kwenye vyoo vya kulipia, hapa hapafai,” mmoja wa wanachuo hao
aliiambia OFM na kuomba hifadhi ya jina lake.
Wanafunzi
hao ambao walitoa ushirikiano wa kutosha kwa makachero wetu, pia
walisema majengo mengi yanayotumiwa kama mabweni yao ya kulala,
yamechakaa na hivyo kuwafanya wawe na hofu kubwa, kwani yanaweza
kuanguka wakati wowote.
WANAFUNZI WA UDAKTARI MUHIMBILI HATARINI
Reviewed by crispaseve
on
06:02
Rating:
Post a Comment