Header AD

CWT YAITAKA SERIKALI KUTATUA KERO ZOTE ZA WALIMU.



1.       Rais wa chama cha walimu Tanzania Gratian Mukoba akielezea kwa kina masuala ya walimu kwa waandishi wa habari ambao hawapo pichani jijini Dar es salaam.(Picha na Kenneth John)

R      Rais wa chama cha walimu Tanzania Gratian Mukoba akifafanua kuhusiana na madai wanayoidai serikali yapatayo shilingi bilioni 40(Picha na Kenneth John)


1.       Rais wa chama cha walimu Tanzania Gratian Mukoba akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wanahabari ambao hawapo pichani mapema leo (Picha na Kenneth John)

R     Rais wa chama cha walimu Tanzania Gratian Mukoba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ambao hawapo pichani(Picha na Kenneth John)

      
      Na Kenneth John,Dar
  

     Chama  cha  walimu  Tanzania  (CWT)   kimeitaka  serikali    kuhakikisha , ifikapo  mwisho  mwa  mwezi   February  2014,   kero  za  walimu  zote  zinapatiwa  zimepatia  ufumbuzi,vinginevyo  chama  kitakuwa  tayari   kutangaza  mgogoro  na  serikali  na  kuhakikisha  wanaitisha  baraza   la  dharula  ili  kuamua  hatua  za  kuchukua  kwa  lengo  la  kupata  haki    stahiki  ndani  ya  mwaka  huu  wa  fedha.
     Hayo  yamesemwa  mapema  leo  na  Rais  wa  chama  hicho,  Gratian  Mukoba  ambapo  amesema  kuwa   serikali  katika  vikao  vyake  na  chama  hicho  ilisema  kuwa  ifikapo  Februari  mwaka  huu   italipa  madai  yote  ya  walimu  yanayohusiana  na  malimbikizo  ya  mishahara  yapatayo   shilingi  Bilioni  40,  Lakini  cha  kusikitisha  katika  kikao  cha   tarehe  4  mwezi  huu   serikali  imeonekana  kubadili  ahadi  yake,  na  badala  yake  imekuja  na  hoja  mpya  na  kusema    kuwa  madeni  hayo   yatalipwa  taratibu   kwasababu   ya  kuhitajika  umakini  katika  kutumia   mfumo  mpya   wa  kielektroniki   wa   kuingiza   madeni   ili   yalipwe.
 
    Aidha  Mukoba  alisema  kuwa ,  kuhusu  suala   la   nyongeza  ya  mshahara ,  hakuna  chochote  ambacho   kimeshapatikana,  pamoja  na  kufanyika  kwa  vikao   mbalimbali  vya  majadiliano   ya  mishahara   ambavyo  vilishafanyika    kutokana  na  maagizo   ya  mahakama  ya    Division   ya  Kazi   ya  mwaka   2012.
   “Baraza  liliniagiza  kuwa   ikifika   mwishoni  mwa   mwezi  wa  pili  majadiliano  hayo  yawe  yamekamilika .Izingatiwe   kuwa  muda  wa  notice   ambao  serikali  ilipewa   na  CWT  uliisha   Januari  5.”Alisema  Mukoba.
    Hata   hivyo  Mukoba  aliendelea   kubainisha  kuwa  serikali  iliahidi    ifikapo   Februari  mwaka  huu   suala  la  kuhusu  majadiliano   ya    nyongeza   ya  mshahara   yatakuwa   yamekamilika,  jambo   ambalo  hadi  sasa   hakuna  chochote  kilichopatikana.  
    Akizungumzia    suala   la  upandishwaji  wa  madaraja  kwa  walimu  Mukoba  alisema  kuwa   serikali  haikufanya  maandalizi   mazuri   katika  mfumo  wa   (OPRAS ) ambao  ni  mfumo   wa  kutathimini   upandishwaji   wa  vyeo  kwa  walimu  ,  kwani   hadi   kufikia   Februari   4   mwaka  huu   ni  mikoa   12   tu     ambayo  nayo  si  kwa  wilaya   zake  zote   ndio  walimu   wamepandishwa  madaraja,   na   huku  mikoa   13   yote   iliyobaki    ilielezwa  kuwa  zoezi  la   kuwapandisha  madaraja    linaendelea.Aidha  Mukoba  aliendelea  kusema    kwa   sura   hiyo  kinachoonekana   ni  zaidi  ya   nusu  ya  mikoa   yote   walimu   wake  hawajapandishwa   madaraja,   na   hadi   sasa    serikali  bado  haijaweka  bayana  ni  lini   walimu  katika   mikoa    iliyobaki   watakuwa   wamepandishwa   madaraja  yao.
CWT YAITAKA SERIKALI KUTATUA KERO ZOTE ZA WALIMU. CWT YAITAKA SERIKALI KUTATUA KERO ZOTE ZA WALIMU. Reviewed by crispaseve on 13:01 Rating: 5

No comments

Post AD