BREAKING NEWWZZZZ:MBUNGE WA CHADEMA AKAMATWA NA JESHI LA POLSI IRINGA AKITUHUMIWA KUGAWA FEDHA KWA WANANCHI
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza na wanahabari
jioni ya leo mara baada ya tukio hilo la kukamatwa kwa Mbunge wa CHADEMA
akigawa fedha kwa wanakijiji siku moja kabla ya uchaguzi
kufanyika.Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika kesho siku ya
jumapili,ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Ikiwa
imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la
Kalenga,Iringa Vijijini,Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili amekamatwa
jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini
akigawa Fedha kwa wanakijiji hao,akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa
kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya
jumapili.
Pichani
shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akielekezwa sehemu ya
kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni
ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata
ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura
kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.
Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.
Mbunge
wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara
baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya
Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji
Gari
ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa
kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi
wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria.
BREAKING NEWWZZZZ:MBUNGE WA CHADEMA AKAMATWA NA JESHI LA POLSI IRINGA AKITUHUMIWA KUGAWA FEDHA KWA WANANCHI
Reviewed by crispaseve
on
03:03
Rating:
Post a Comment