Header AD

KAMPENI ZA CCM CHALINZE ZAZIDI KUSHIKA KASI


 Mbunge a Jimbo la Mchinga,Mh. Said Mtanda (kulia) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014,wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (wa pili kushoto walioketi).Picha na Othman Michuzi,Chalinze.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014.Katika Mikutano yake kwenye Vijiji vya Mindukene, Msigi na Kisanga ndani ya Jimbo hilo,Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo.
Wananchi wa Kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze wakimsikiliza kwa makini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akilakiwa na wanakijiji wa Kijiji cha Msigi Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze  Machi 18,2014.
KAMPENI ZA CCM CHALINZE ZAZIDI KUSHIKA KASI  KAMPENI ZA CCM CHALINZE ZAZIDI KUSHIKA KASI Reviewed by crispaseve on 00:00 Rating: 5

No comments

Post AD