KANUMBA THE GREAT FOUNDATION KUMUENZI MAREHEMU STEVEN KANUMBA.
Uzinduzi wa taasisi ya marehemu Steven Kanumba ijulikanayo
kwa jina la Kanumba The Great Foundation utafanyika Aprili 7 kwenye
ukumbi maarufu wa Dar Live uliopo Mbagala, jijini. Uzinduzi
huo utaenda sambamba na maadhimisho ya miaka miwili tokea kufariki kwa
marehemu Kanumba ambaye alifariki dunia Aprili 7.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mama mzazi wa
marehemu Kanumba, Flora Mtegoa alisema kuwa wameamua kuanzisha taasisi
hiyo ili kuendelea kumuenzi mtoto wake na kuendeleza kile ambacho
alikuwa akikifanya wakati wa uhai wake.
Alisema kuwa taasisi yao itajihusisha na utoaji wa elimu,
kusaidia watoto yatima, kuibua vipaji vya waigizaji chipukizi na
kuviendeleza na mambo mbali mbali ya jamii na tasnia ya filamu na
muziki.
“Kwa njia hii, jamii itaendelea kumkumbuka kila siku na si
kusubiri maadhimisho ya siku yake aliyokufa tu, siku hii (Aprili 7 kila
mwaka) itabaki kuwa ya kukumbukwa, lakini tutajihusisha na mambo mengine
ya maendeleo na kusaidia jamii,” alisema Mtegoa.
Alisema kuwa wameamua kuipa jukumu kampuni ya Vannedrick
Tanzania Limited kufanya shughuli za uzinduzi wa taasisi hiyo kutokana
na uadilifu wao na kuvunia na jinsi inavyojihusisha na mambo mbali mbali
katika jamii.
Mkurugenzi kuu wa Vannedrick Tanzania Limited Frederick
Mwakalebela alisema kuwa siku hiyo mbali ya kuwa na Red Carpet, pia
kutakuwa na burudani mbali mbali za muziki wa dansi, muziki wa kizazi
kipya na vichekesho kutoka kwa wasanii maarufu hapa nchini.
Alisema kuwa kutakuwa na maonyesho ya filamu mbali mbali za
marehemu Kanumba ikiwa pamoja na script alizokuwa akiandika yeye
mwenyewe, nyimbo alizotunga na vingienvyo.
“Pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Movie
ambao wameanza maandalizi kwa ajili ya siku hiyo maalum kwa waigizaji na
mashabiki wa filamu nchini, tunawamba wadhamini wajitokeze ili
kufanikisha siku hiyo,” alisema.
-bongomovies.com
KANUMBA THE GREAT FOUNDATION KUMUENZI MAREHEMU STEVEN KANUMBA.
Reviewed by crispaseve
on
15:31
Rating:
Post a Comment