ARNOLD SCHWARZENEGGER AONGELEA UJIO WA FILAMU MPYA YA TERMINATOR ITAKAYOTOKA 2015.
Muigizaji wa muvi za action na aliyekuwa gavana wa jimbo la
California Marekani, Arnold Schwerzenegger(67) amesema kwamba anatarajia
kuigiza kwenye filamu mpya ya ‘Terminator’ itakayoanza kutazamwa rasmi
kwenye kumbi za sinema Julai 1 mwaka 2015.
Aliyasema hayo akiwa kwenye tamasha lake la michezo ‘Arnold
Sports Festival’ lilofanyika katika mji wa Columbus na kuwataka
mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani wataanza rasmi shughuli za
utengenezaji wa filamu hiyo ifikapo mwezi April mwaka huu.
”Tutaanza shughuli za utengenezaji katikati au mwishoni mwa
mwezi wa nne na tutacheza katika mji wa New Orleans baadhi ya vipande na
San Francisco na kwa kiasi kidogo Los Angels lakini sehemu kubwa
itakuwa ni New Orleans, natazamia matarajio makubwa kama unavyofahamu
kipindi cha mwisho nilipocheza kwenye filamu ya Terminator nilikuwa
tayari gavana kwaiyo nisingeweza kuwa kwenye hii filamu ila kwa sasa
nimerudi tena na waandaaji wa filamu hii wamefurahishwa kuwa na mimi kwa
mara nyingine, Skripti ni nzuri na hivyo natazamia zaidi kwenye filamu hii mpya”, alisema Staa huyo .
Awali Schwerzenegger aliwahi kuigiza kwenye filamu za
‘Terminator’ zilizokuwa na muendelezo ikianzia na ‘Terminator
Judgement Day(1991)’, Rise of the machine(2003) na ile ya mwaka 2009
‘Terminator Salvation’. kama wewe ni mdau wa movie hii sio ya kukosa.
ARNOLD SCHWARZENEGGER AONGELEA UJIO WA FILAMU MPYA YA TERMINATOR ITAKAYOTOKA 2015.
Reviewed by crispaseve
on
15:30
Rating:
Post a Comment