YANGA YALOWA MISRI, YAFUNGWA NA AL AHLY KWA MIKWAJU YA PENALTI 4 -3 .
Kikosi cha jagwani, Young Africans kimekubali kung’oka kiume
mbele ya mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri iliyoibuka mshindi kwa
mikwaji ya penalti 4 – 3 na hivyo kuwatoa wawakilishi hao pekee wa
Tanzania kwenye mashindano ya klabu bingwa ya Afrika.
Katika mchezo huo, al ahly iliweza kujipatia bao lake la
kwanza mnamo dakika ya 70 na kufanya matokeo kuwa 1 – 0 yaliyoifikisha
hatua ya matuta ambapo penalti ya Said Bahanuzi ilishindwa kuzaa
matunda baada ya kutoka nje na kuifanya Al ahly kusonga mbele katika
hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Afrika.
YANGA YALOWA MISRI, YAFUNGWA NA AL AHLY KWA MIKWAJU YA PENALTI 4 -3 .
Reviewed by crispaseve
on
15:27
Rating:
Post a Comment