DUH! HII NDO LIST YA WASANII WENYE NYOTA ZA NGONO......Maalim Hussein Yahya!
Makubwa! Mtabiri
maarufu Bongo, Maalim Hussein Yahya ameanika nyota za baadhi ya mastaa
wa Bongo katika kipengele cha mapenzi au ngono, Risasi
Jumamosilimesheheni.
Akizungumza na
mapaparazi wetu katikati ya wiki hii ofisini kwake Magomeni-Mwembechai
jijini Dar, Maalim alitumia saa kadhaa kuangalia nyota ya mmoja baada ya
mwingine na kueleza sifa zao katika sekta ya uhusiano na tendo la ndoa.
Baadhi ya mastaa
alioweza kuwasoma nyota zao kirahisi ni pamoja na ‘kichaa’ wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, waigizaji Wema Sepetu, Vincent
Kigosi ‘Ray’, Aunt Ezekiel, Steven Jacob ‘JB’, Jacqueline Wolper,
Blandina Chagula ‘Johari’ na wengine.
ALIANZA NA WEMA
Akimzungumzia
Wema aliyezaliwa Septemba 28, Maalim alisema nyota yake ni Mizani hivyo
ana tabia zifuatazo katika masuala ya mapenzi:
“Kwanza yeye (Wema) na Diamond nyota yao ni moja hivyo mambo yao mengi yanafanana.
“Wanapenda kuwa kwenye ulimwengu wa mapenzi na mahaba wakati wote. Wanathamini sana masuala ya ngono kuliko maisha mengine.”
NDOA NA DIAMOND
“Hawa watakuwa watu wa kuachana na kurudiana mpaka watakapofunga ndoa ya kifahari hapo baadaye.
“Kuhusu mambo
mengine kinyota ni kwamba wana sifa ya uongozi, wanapenda kuwa huru na
kujitegemea. Wanapenda kuheshimika kwenye jamii na ni wacheshi, wana
hekima na diplomasia.”
KUHUSU RAY
Kwa upande wake Ray ambaye amezaliwa Mei 28, Maalim alisema nyota yake ni Mapacha.
Akimchambua kinyota kuhusu masuala ya mapenzi, alisema:
“Akimpenda mwanamke ana uwezo wa kumpa chochote, kimawazo na kila kitu, anaweza hata kuhamia nyumbani kwa mwanamke huyo.
Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa na mpenzi wake Chuchu Hans.
“Ila ni mtu anayechoka haraka na hawezi kudumu kwa muda mrefu kwenye penzi na mwanamke mmoja tu.
“Pia anapenda kuwa na mapenzi ya siri siku zote. Hata akioa ni lazima ataendelea kuwa na mwanamke wa nje ‘nyumba ndogo’.
“Mbali na masuala
hayo, ni mtu mwenye hisia kali sana ambapo hukasirika upesi. Ni mtu
mwenye uwezo wa kujieleza na kuzungumza, ana ushawishi mbele za watu.”
AUNT EZEKIEL NAYE
Akimchambua Aunt Ezekiel ambaye alizaliwa Oktoba 27, mtabiri huyo alisema nyota yake ni Nge.
“Kinyota, ni mtu mwenye ‘muwashawasha’ wa mapenzi, anapokuwa na hasira tu hupenda kuzimaliza kwa kufanya tendo la ndoa.
“Ni msiri sana.
Ana wapenzi wengi lakini kwa siri. Kwake tendo la ndoa ni ishu muhimu
sana katika maisha yake hasa ikizingatiwa kuwa, nyota ya Nge inatawala
sehemu za siri.
“Kwa mwenye moyo
mdogo, asifanye mapenzi na mtu mwenye nyota hii kwani atajuta maisha
yake yote. Lakini hayumbi na hakubali kushindwa hata kwa jambo ambalo
halitamharibia popote.”
JB & WOLPER
Kwa upande wa JB
aliyezaliwa Desemba 4, Wolper aliyezaliwa Desemba 6, Maalim alisema wote
wana nyota moja inayofanana ya Mshale. Anaichambua nyota hiyo hivi:
“Wanapenda
kufanya ngono kwa muda mrefu, hivyo mwanamke au mwanaume atakayekuwa nao
kimapenzi lazima awe amekula akashiba vizuri kabla ya tendo lenyewe.
“Wapenzi wao wanapowaonesha dalili ya kuwapenda sana basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu.
“Wanapoingia
katika mapenzi wanakuwa waaminifu na wanakolea vilivyo. Mara nyingi
wanapenda sana kuwa na wapenzi wapya, lakini hawapendi mapenzi ya kudumu
kwa sababu yanawanyima uhuru.
NYOTA YA JOHARI SASA
Akimzungumzia Johari aliyezaliwa Agosti Mosi, mtaalam huyo alisema nyota yake ni Simba. Anasema:
“Kinyota ana tatizo la kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani ni mtu anayeumia.
“Mara nyingi hujipa hisia za kupendwa na mpenzi wake kama anavyompenda yeye.
“Ni mkarimu lakini ni jeuri, anapenda sana kuonea wenzake. Anapenda kujionesha na humharibu mpenzi wake.”
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
DUH! HII NDO LIST YA WASANII WENYE NYOTA ZA NGONO......Maalim Hussein Yahya!
Reviewed by crispaseve
on
15:24
Rating:
Post a Comment