KESI YA MBUNGE WA IRINGA MJINI (CHADEMA) YAAHIRISHWA MPAKA APRIL 9
picha kwa hisani ya mitandao ya kijamii.
Mbunge wa jimbo la
Iringa mjini Mh.PETER MSIGWA kwa mara nyingine amefikishwa
leo katika mahakama kuu ya mkoa , kufuatia tuhuma
inayomkabili ya kufanya vurugu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani
katika kata ya nduli manispaa ya iringa.
Tukio hilo limetoke
tarehe 6 ya mwezi wa pili ambapo SALUM KEITA mjumbe
wa kampeni hizo kupitia chama cha mapinduzi alidai kufanyiwa
vurugu na mbunge wa jimbo la iringa mjini kwa kumpiga.
Kesi hiyo imesomwa leo katika
mahakama ya wilaya ya Iringa mbele ya jaji ALOYCE MASUA na
kesi hiyo imeahirishwa na kutajwa kusikilizwa
tarehe 9 ya mwezi wa 4
mwaka huu.
KESI YA MBUNGE WA IRINGA MJINI (CHADEMA) YAAHIRISHWA MPAKA APRIL 9
Reviewed by crispaseve
on
09:53
Rating:
Post a Comment