KKKT: Nawaita waumini Tamasha la Pasaka
KANISA
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mkoa wa Morogoro limetoa wito
kwa jamii kuungana na Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama katika
kipindi hiki cha Pasaka kutumia kidogo ambacho Mungu amewajalia
kuwakumbuka wenye mahitaji maalum kama vile walemavu, wajane na yatima.Wito
huo umetolewa na Mchungaji Raymond Dunia wa kanisa hilo akiwa na nia ya
kuwakumbusha Wakristo kuwa na moyo wa kujitolea hasa kwa wenye mahitaji
maalum.
Anasema
kuwa lengo la Msama kusaidia jamii kupitia matamasha ya nyimbo za
injili ni lengo zuri kwa kipindi hiki cha Pasaka, kwani ni wakati wa
ukombozi kwa waliokandamizwa, Pasaka ni furaha kwa walio wahitaji, pia
Pasaka ni amani kwa watu wenye mashaka ya maisha yao.
Anaongeza
kwa kusema kuwa kupitia matamasha ya nyimbo za injili watu wengi
wanaokolewa, hivyo ni njia mojawapo ya kusababisha watu waokolewe. “Wapo
watu wenye mipango bora ya kusaidia jamii, lakini wanapofanikiwa
wanajihudumia wenyewe. Msama awe mfano mwema katika kuisaidia jamii ili
kutimiza lengo la Kristo aliyesema, “Wenye afya hawahitaji tabibu ila
walio hawawezi,”” alisema.
Hata
hivyo mchungaji Dunia amesema kuwa wapo wanaotumia fedha nyingi kwa
kuandaa sherehe katika sikukuu ya Pasaka huku wengine wakihangaika
kutafuta angalau mlo mmoja wa siku, hata katika kipindi cha sikukuu kama
hiyo, lakini wakumbuke kuwa ni vyema kwenda kuwatia moyo kuwafariji
wale wanaolea wenye uhitaji maalum vituoni.
Aliongeza
kwa kumtia moyo Msama aendelee na moyo huo wa imani wa kuwasaidia
wasiojiweza kwa kuwa anayetoa atazidishiwa mara dufu, kwa kuwa yeye yu
miongoni mwa wachache wenye moyo wa kusaidia wahitaji hao.
Anatoa
wito kwa mashabiki na waumini wajitokeze kwa wingi kuhudhuria matamasha
hayo kwa kuwa kupitia nyimbo za injili watabarikiwa na hata kujifunza
neno la Mungu. Pia aliwapongeza waimbaji wa nyimbo za injili kwa kuwa
wao wamekuwa ni njia nyingine ya kutangaza neno la Mungu na kupitia wao
watu wengi wanaokolewa. Hivyo wajue kuwa wao pia ni kioo cha jamii,
jamii inahitaji kujifunza kutoka kwao
.
Matamasha
hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika mikoa tofauti yamekuwa ni moja
ya njia pekee ya kupunguza uhalifu na kuongeza kipato cha
wafanyabiashara wanaofanya biashara maeneo ya karibu na yanapofanyika
matamasha hayo.Hata hivyo Msama ana nia ya kujenga kituo cha kusaidia
wahitaji hao ambacho kitasaidia maeneo mbalimbali kama kuwasaidia
wahitaji wenye kipaji cha uimbaji.
Pamoja
na hayo Msama anaiomba jamii, ikae tayari kusubiri matamasha hayo
yanayosubiriwa kwa hamu katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na mashabiki
wa nyimbo za injili kujitokeza kwa wingi kwa kipindi hicho cha
matamasha ili kuweza kumsapoti kutimiza lengo lake la kusaidia wahitaji
hao.
KKKT: Nawaita waumini Tamasha la Pasaka
Reviewed by crispaseve
on
08:24
Rating:
Post a Comment