MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI RUKWA, WANAWAKE WAASWA KUJIENDELEZA KIELIMU KUSHIKA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NCHINI
Maadhimisho
hayo yalianza kwa maandamano mbalimbali yaliyopita mbele ya meza kuu
ambayo mgeni rasmi alikua Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta
akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Viongozi mbalimbali wa meza kuu wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi
Kimanta (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga Mhe. Maembe (wa pili kushoto) na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa
Rukwa Francis Kilawe (wa nne kushoto) wakionyesha ishara ya kupokea
maandamano hayo. Wengine kutoka kulia ni Makatibu Tawala wa Wilaya za
Nkasi, Kalambo na Sumbawanga.
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta (wa nne kushoto) na viongozi
wengine wa Serikali Mkoani Rukwa wakipokea maelezo ya bidhaa mbalimbali
kutoka kwa wajasiriamali waliofanya maonyesho ya bidhaa zao katika
sherehe hizo. Pamoja na maonyesho hayo huduma za kupima VVU kwa hiyari
pia zilitolewa sambamba na michezo mbalimbali na nyimbo za kunogeza
sherehe hizo.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta akihutubia hadhara iliyohudhuria
maadhimisho hayo ambapo amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika
kujiendeleza kielimu waweze kushika nafasi mbalimbali za uongozi kama
walivyofanikiawa viongozi wengine wanawake hapa nchini na barani Afrika.
Aliwatolea mfano baadhi ya viongozi hao kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia Stella Manyanya, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Anna Makinda n.k.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimkabidhi Bi Bahati Mgimwa Afisa
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Wilaya ya Sumbawanga zawadi
mbalimbali zilizotolewa na Dawati la Jinsia Mkoa wa Rukwa kwa watoto
wanaoishi katika mazingira magumu katika Kijiji cha Kalambanzite
Wilayani Sumbawanga. Zawadi hizo zenye thamani ya shilingi laki tatu ni
Sabuni, Sukari, Chumvi na nguo.
MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI RUKWA, WANAWAKE WAASWA KUJIENDELEZA KIELIMU KUSHIKA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NCHINI
Reviewed by crispaseve
on
21:41
Rating:
Post a Comment