MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI UPIMAJI WA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA AKINA MAMA HAPA NCHINI.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akizindua rasmi upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi wakati wa kilele cha siku ya wanawake duniani katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Nyamagana huko Mwanza
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi aliwakabidhi Waganga wakuu wa mikoa ya Mwanza, Iringa, Mbeya na Mara vifaa vya kupima saratani hiyo. Pichani Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Valentino Bangi mkoba wenye vifaa vya upimaji.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Nestory Masalu kutoka hospitali ya Rufaa ya Bugando ambaye alikuwa akiwapima akina mama katika kituo cha Afya cha Buzuruga kilichoko katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi katika uwanja wa Nyamagana na kutembelea kituo hicho ambapo wanawake wengi walijitokeza kwa ajili ya kupima. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI UPIMAJI WA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA AKINA MAMA HAPA NCHINI.
Reviewed by crispaseve
on
21:38
Rating:
Post a Comment