MUUNGANO WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YANAYOTETEA HAKI ZA WANAWAKE YANAYOTETEA HAKI ZA WANAWAKE WASHEREKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI.
Kutoka
kushoto ni Miss Tanzania 2013 Happy Watimanywa , Dk. Agnes Nyomola
kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye ni Mtaalam wa mambo ya
Sayansi, na Specioza Rweyemamu ambaye ni Ispecta katika mambo ya anga
katika Mamlaka wa usafiri wa Anga Tanzania, ambao ndio walikuwa wasemaji
katika sherehe hizo
Dk. Agnes Nyomola kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye ni Mtaalam
wa mambo ya Sayansi akizungumza na wanafunzi kutoka shule mbalimbali
jijini Dar es salaam waliofika katika sherehe hizo za siku ya wanawake
Duniani na kuwasihi kupenda masomo ya Sayansi kutokana na kwamba kwa
sasa Dunia imebadilika na tunapo elekea ni Karne ya Sayansi na
Teknolojia, amewasihi pia wasichana kupenda masomo hayo akiamini kuwa
wanaweza na kwamba ni Fursa muhimu sana kwao.
Specioza
Rweyemamu ambaye ni Ispecta katika mambo ya anga katika Mamlaka wa
usafiri wa Anga Tanzania akizungumza na wanafunzi pamoja na wageni
waalikwa mbalimbali hasa wanafunzi na kuwaasa kuwa wanatakiwa kuwa mfano
wa kuigwa katika jamii na kusoma kwa bidii kwani hakuna kisicho
wezekana kila mtu anaweza, pia amewasihi wasichana hasa wadogo kupenda
kusoma zaidi ili waje kuwa viongozi wa baadae.
Wakili
wa Mahakama Kuu Modesta Mahiga akizungumza na wanafunzi waliofika
katika Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Chuo Kikuu Dar es salaam na
kuwahimiza wanafunzi hasa wakike wanaokuwa wasikimbilie katika mambo
makubwa lakini wakazane na masomo ili kupata kufanikiwa zaidi.
Miss
Tanzania 2013 Happy Watimanywa akiongea na wanafunzi, alisisitiza sana
wanafunzi wenzake wa kike kuwa wanatakiwa kusoma kwa Bidii ili kuweza
kuja kufanikiwa katika mambo yao ya mbeleni, aliongeza kuwa mtoto wa
kike ndio taifa la kesho na kiongozi wa kesho hivyo ni lazima wakazane
sana katika masomo yao na kuichukulia siku ya leo kama changamoto na
chachu kwao ya kujibidisha zaidi.
Mwenyekiti
wa Muunganiko wa mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotetea haki za
Wanawake Tanzania Bi. Juliana Bwire akitoa neno la Shukurani kwa
wasemaji wote waliokuwa wakizungumza kila mmoja kwa wakati wake , pia
kuwashukuru wote waliofika katika Sikukuu hiyo ya Mwanamke Duniani.
Jane
Mrema Mshauri wa Jinsia kutoka Shirika la Plan International akielezea
nia yao kubwa ya kushiriki katika Sherehe hizo Leo.
<![endif]-->Gloria
Chambo mwanachama wa chama cha Muunganiko wa mashirika yasiyo ya
Kiserikali ambaye ndiye alikuwa mshereheshaji wa Siku hiyo ya wanawake
akizungumza Jambo wakati wa Sherehe hizo na kuongoza ratiba hiyo.
MUUNGANO WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YANAYOTETEA HAKI ZA WANAWAKE YANAYOTETEA HAKI ZA WANAWAKE WASHEREKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI.
Reviewed by crispaseve
on
21:35
Rating:
Post a Comment