MISS TABORA 2012 ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO NA KUFURAHIA SIKU YAKE YA KUZALIWA
Mrembo
Sarah Paul aliposhiriki furaha yake ya siku ya kuzaliwa na watoto wa
kituo cha TZ 820 FPTC NG'AMBO STUDENT CENTER - Kilichopo Tabora.
Kila mmoja alipata nafasi ya kufurahia keki iliyoandaliwa maalumu kwa watoto hao.
Baadhi ya vitu alivyowaandalia watoto hao na kuvikabidhi kwenye shirika hilo.
Sarah
Paul, mshindi wa shindano la urembo la Redds Miss Tabora 2012, ambaye
pia mwaka jana alishiriki katika shindano hilo hadi kufikia fainali za
Miss Tanzania.
****
Leo
katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa amefanikiwa kuwatembelea
watoto wanakusanywa na kanisa la FPCT NG'AMBO wanaopewa msaada na
Shirika la Compassion International Tanzania na kuwasaidia watoto
wanaoishi katika mazingira magumu. Watoto hawa wanakusanywa kwa lengo la
kuwatoa na kuwakomboa umaskini wa kiuchumi, kijamii, kimwili na kiroho
na kuwawezesha waje wawe watu wazima wanaojua wajibu wao na kujitegemea.
Pia
huwalipia ada, huwauguza na kuwapeleka hosipitali wanapoumwa,
huwafundisha ujasiriamali n.k Aliyasema Suleiman H. Halletu mkurugenzi
wa kituo kinachoitwa TZ 820 FPCT NG'AMBO STUDENT CENTER na kuongeza kuwa
wana watoto 254 katika kituo chao.
MISS TABORA 2012 ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO NA KUFURAHIA SIKU YAKE YA KUZALIWA
Reviewed by crispaseve
on
13:36
Rating:
Post a Comment