Header AD

MO aapishwa rasmi Bungeni


IMG_9709
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Singida mjini, Ndg. Mohammed Dewji ( wa pili kushoto) akiteta jambo na baadhi ya Wajumbe wenzake wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo wakati wa sherehe fupi za kuapishwa kwa wajumbe hao.
IMG_9729
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Singida mjini, Ndg. Mohammed Dewji akielekea kula kiapo cha kulitumikia Taifa Bunge la Katiba.
IMG_9731
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Mohammed Dewji akila kiapo mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Samwel Sitta mjini Dodoma.
IMG_9739
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Mohammed Dewji, akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Samwel Sitta mjini Dodoma.
IMG_9741
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Samwel Sitta , akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Mohammed Dewji.
MO aapishwa rasmi Bungeni MO aapishwa rasmi Bungeni Reviewed by crispaseve on 03:07 Rating: 5

No comments

Post AD