Header AD

NISHER AWAHASA WATAYARISHAJI WA VIDEO NCHINI KUPENDA KUUMIZA VICHWA.



Mtayarishaji wa muongozaji na video  anayekuja kwa kasi kutoka Arusha, Nisher,  amewaambia watu wanaomtaka aache kufanya Colour Corection na kuacha mazingira halisi za video zake waache kupenda vitu simple na kutakiwa kuumiza vichwa,
Akitolea mfano wa video mpya aliyofanya ya mwanamuzki Baraka Prince alieleza endapo  angefanya mtayarishaji mwingine, angelaumu Location za Tanzania  ngeitumia hiyo picha ya Before kama ilivyo kwenye video yake na angeweka color ya ajabu ilikuyasaidia hayo majani yarudi but bado isingeonekana professional.
”Kuna watu wajuaji wananiambiaga niache video zangu Natural nisifanye colour corrections wala grading…mimi sio mjuaji ila nadhani napenda tu kuumiza kichwa changu kidogo zaidi, isitoshe najifunza kila siku… sababu kama picha hii kwamfano (kutoka kwenye Video mpya Ya BARAKAH) ingekua mtu mwingine angefanya yafuatayo ,1. Angelaumu Location za Tanzania 2. Angeitumia hiyo picha ya Before kama ilivyo kwenye video yake, 3. Angeweka color yaajabu ilikuyasaidia hayo majani yarudi but bado isingeonekana professional. Ushauri tu… Tusipende vitu simple! UMIZENI VICHWA!!!”, aliandika dairekta huyo kupitia ukurasa wake wa FACEBOOK.
Pichani juu ni moja ya kipande kilichopo kwenye video aliyotengeneza Nisher ya Barakah akitolea mfano kabla na baada.
NISHER AWAHASA WATAYARISHAJI WA VIDEO NCHINI KUPENDA KUUMIZA VICHWA. NISHER AWAHASA WATAYARISHAJI WA VIDEO NCHINI KUPENDA KUUMIZA VICHWA. Reviewed by crispaseve on 14:34 Rating: 5

No comments

Post AD