Tafrija ya Kuwapongeza Mhe. Samuel Sitta na Mhe Samia Suluhu.kwa Ushindi wao.
Mwenyekiti wa Bunge
Maalum la Katiba Mh. John Samuel Sita akitoa neno la shukrani mara
baada ya Tafrija fupi ya kupongezwa kwake yeye na Makamu wake Mh. Samia
Suluhu hapo Chinese Restaurant Mjini Dodoma.
Mke wa Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza katika
Tafrija fupi ya kupongezwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge
Maalum la Katiba Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mh. Moh’d Aboud Moh’d
akizungumza wakati wa tafrija hiyo ya kuwapongeza Mwenyekiti na Makamu
wake kwa kuchaguliwa kuliongoza Bunge Maalum la Katiba Tanzania ,tafrija
hiyo imefanyika katika hoteli ya ya Dodoma hoteli Mgahawa wa Kichina.
Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania ambae pia ni Waziri wa
Nchi anayeshughulikia Muungano Mh.Samia Suluhu Hassan Kushoto akiwa
pamoja na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman
Iddi katika Tafrija ndogo ya kuwapongeza Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
wa Bunge hilo mara baada ya kuchanguliwa kuliongoza Bunge hilo
linaloendelea kukutana Mjini Dodoma.
Washiriki
wa Tafija fupi ya Kupongezwa kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba
Mh. John Samule Sita na Makamu wake Mh. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika
katika Mkahawa wa China uliomo ndani ya Dodoma Hoteli.(Picha na Hassan
Issa -OMPR)
Tafrija ya Kuwapongeza Mhe. Samuel Sitta na Mhe Samia Suluhu.kwa Ushindi wao.
Reviewed by crispaseve
on
21:35
Rating:
Post a Comment