PICHA: KAMPENI YA KUPAMBANA NA HOMA YA INI YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk. Meshack Shimwela, akielezea madhara ya ugonjwa wa Homa ya Ini.
Shigongo akiwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kupambana dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Ini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akiandika huku akitafakari jambo wakati wa uzinduzi huo.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe akielezea umuhimu
wa wananchi kupima virusi vya ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B).
Meza kuu wakibadilishana mawazo.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakifuatilia uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akizindua rasmi kampeni ya kupambana na ugonjwa hatari wa Homa ya Ini.
Ini likiwa salama kabla ya kushambuliwa na virusi vya Hepatitis B.
...Ini baada ya kushambuliwa na virusi vya Hepatitis B.
...Ini lenye kansa.
Shigongo akimpongeza mgeni rasmi, Said Mecky Sadick baada ya uzinduzi.
Mmoja wa mapaparazi akijiandaa kuchukua matukio katika uzinduzi huo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliofanikisha kampeni hiyo.
Mgeni rasmi akiagana na Eric Shigongo baada ya zoezi la uzinduzi kukamilika.
Wananchi wakipima virusi vya Hepatitis B vinavyosababisha ugonjwa wa Homa ya Ini.
Shigongo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ) baada ya uzinduzi.
--
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick amezindua rasmi kampeni ya
kupambana na Ugonjwa wa Homa ya Ini katika Hospitali ya Amana, Ilala
jijini Dar es Salaam.
Kampeni
hiyo imeandaliwa na Kampuni ya Global Pulishers Ltd wakishirikiana na
Wizara ya Afya, SD Africa, Sanofi, Megra Clinic, Damu Salama na Tamsa.
Katika
uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka wadau
mbalimbali kuonyesha ushirikiano katika kupambana na ugonjwa huo hatari
kuliko HIV huku akiwaasa wananchi kuacha vitendo vinavyoweza kuleta
maambukizi ya ugonjwa huo unaombukizwa kwa njia sawa na za HIV.
PICHA ZOTE NA GPL
PICHA: KAMPENI YA KUPAMBANA NA HOMA YA INI YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR
Reviewed by crispaseve
on
22:26
Rating:
Post a Comment