TAMASHA LA PASAKA KUTIMIZA MIAKA 14 TANGU KUANZISHWA KWAKE NA MSAMA PROMOTIONS YA JIJINI DAR
TAMASHA
la Pasaka mwaka huu limetimiza miaka 14 tangu kuasisiwa kwake na
Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam imekuwa ikijiongezea
umaarufu na kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya
maadhimisho ya Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa
kiroho kupitia matamasha hayo.
Umaarufu
wa matamasha hayo pamoja na mambo mengine, unatokana na ukweli kuwa
yamekuwa yakifanyika kwa ubunifu na umakini mkubwa huku kila mwaka
yakiongezeka na kubadili waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa
ndani na nje ya nchi.
Imebainika
kuwa tamasha hilo ni kivutio kwa watu mbalimbali kiasi cha kuwafanya
kila linapoandaliwa Tamasha la Pasaka na Krismasi, Uwanja wa Taifa
uliopo jijini Dar es salaam ambao umekuwa ukitumika kwa kazi hiyo,
kufurika watu nao kutoka wakiwa na mioyo iliyotakasika kupitia nyimbo na
waimbaji hao.
Hapana
shaka kuwa ubunifu huu ndio ulichangia hata Serikali kupitia Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenela Mukangala, kumteua
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, kuwa Mjumbe wa Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA).
Matamasha
haya yanapambanuliwa na wadau mbalimbali ambao wanayaelezea ubora wake
lakini wengi wanasema, yanapata umaarufu na mvuto kwa kuwa washiriki
hususan waandalizi na wasanii (waimbaji), wanajiandaa na kujua
kinachohitajika kwa jamii, hivyo kukiwasilisha kadiri ya mahitaji ya
jamii.
Waimbaji mbalimbali wakiwamo wa kutoka nje ya nchi, wamekuwa wakikonga nyoyo za wananchi kwa kushirikiana vizuri na wazawa.
Sababu
ya Kamati za Maandalizi za Matamasha haya kuleta waimbaji kutoka nje ni
pamoja na hasa, kuleta ladha tofauti kwa nia ya kupata mahubiri au Neno
la Mungu kwa ladha tofauti kutoka kwa waimbaji hao.
TAMASHA LA PASAKA KUTIMIZA MIAKA 14 TANGU KUANZISHWA KWAKE NA MSAMA PROMOTIONS YA JIJINI DAR
Reviewed by crispaseve
on
07:13
Rating:
Post a Comment