WAFANYAKAZI WANAWAKE KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAUNGANA NA WANAWAKE WENZAO KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA UWANJA WA MWEMBE YANGA
Wafanyakazi
Wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiungana na wanawake wenzao
kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga
Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014.
Baadhi
ya wafanyakazi wanawake kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika
maandamano yaliyokuwa yakielekea katika Uwanja wa Mwembe Yanga Mapema
leo Katika Kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani ambapo wafanyakazi
wanawake wa PPF nao waliweza kujumuika na wanawake wenzao katika
kusherehekea Siku hiyo
Wafanyakazi
wa PPF wakiingia katika Uwanja wa Mwembe Yanga huku wakiwa na Bango lao
linalosomeka "Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia, PPF Fao la
Elimu - Linazingatia Usawa wa Kijinsia"
Wafanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF (Waliovalia Fulana za Rangi ya Blue) wakiwa
wameketi kwenye eneo lao huku wakifuatilia matangazo yaliyokuwa
yakitolewa katika Uwanja wa Mwembe Yanga wakati wa Maadhimisho ya
Sikukuu ya Mwanamke Dunia.
Baadhi
ya Wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika picha
ya pamoja wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Sikukuu ya Wanawake
Duniani ambayo imefanyika katika Uwanja Wa Mwembe Yanga, Wilaya ya
Temeke, Mkoa wa Dar Es Salaam mnamo Machi 8, 2014
WAFANYAKAZI WANAWAKE KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAUNGANA NA WANAWAKE WENZAO KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA UWANJA WA MWEMBE YANGA
Reviewed by crispaseve
on
21:44
Rating:
Post a Comment