Airtel yazindua whatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia Vifurushi vya yatosha
· Sasa wateja kupata whatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia yatosha bando
kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora
imezindua huduma ya kibunifu itakayowawezesha wateja wake kupata na
kuunganishwa kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Whatsapp na twitter
BURE kupitia huduma ya Airtel yatosha.
Akiongelea
kuhusu huduma hiyo Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Airtel Bi
Beatrice Singano Mallya alisema” sasa ni bure kabisa kwa wateja wetu
wote wa Airtel kuunganishwa na mitandao ya kijamii ya Whatsapp, Facebook
na Twitter. Airtel tunayofuraha kutoa nafasi kwa wateja wetu
kuwasiliana na marafiki na familia kupitia mitandao hii ya kijamii bure
bila makato yoyote, huku tukiendelea kuthibitisha kuwa Airtel Yatosha
ni BABA LAO!”
Aliongeza
kwa kusema mteja yoyote atakayenunua kifurushi cha data cha yatosha
kuanzia sasa iwe ni cha siku, Wiki au Mwezi vifurushi vyao vya internet
vya MB au GB hazitakatwa katika matumizi ya Facebook, Whatsapp na
Twitter na badala yake wataweza kutumia vifurushi vyao vya data kwenye
kuperuzi katika mitandao mingine kama vile YouTube na mingine mingi
kadri ya mahitaji yao”
Akiongea
kuhusu namna ya kujiunga Meneja Masoko wa Airtel Bi Upendo Nkini
alisema” ili kupata Whatsapp, Facebook na Twitter BURE wateja watatakiwa
kupiga *149*99# kisha kuchagua kifurushi kinachowafaa na kuanza kufurahia BURE Whatsapp, Facebook na Twitter”
“Sambamba
na hilo katika kuendeleza ubunifu na kurahisiaha upatikanaji wa
vifurushi vya Yatosha, tumewawezesha wateja wetu kutumia simu za
kununua vifurushi vya yatosha kwa ajili ya marafiki zao familia na
kubaki wakiwa wameunganishwa na kufurahia mitandao hii ya kijamii ya
Whatsapp, Facebook na Twitter BURE, furahia kuunganishwa katika
mawasiliano kupitia mtandao wa Airtel” aliongeza Nkini
Airtel yazindua whatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia Vifurushi vya yatosha
Reviewed by crispaseve
on
05:03
Rating:

Post a Comment