JUSTIN BIEBER KUMSINDIKIZA BONDIA FLOYD ‘MONEY’ MAYWHEATHER KATIKA PAMBANO LAKE LA LEO DHIDI YA MAIDANA
Mwanamuziki
Justin Bieber atamsindikiza kwa mara nyingine tena rafiki yake kipenzi
bondia ‘Floyd Money Maywheather’ katika mpambano wake wa leo usiku
dhidi ya muagentina ‘Marcos maidana’ utakaochezwa katika ukumbi wa MGM
Grand garden Arena mjini Las Vegas marekani.
Maywheather anatamba na rekodi ya kutowahi kupoteza pambano
tangu aanze ngumi za kulipwa. Mashabiki wengi wa masumbwi Duniani
wamekuwa wakijiuliza kama rekodi hiyo itavunjwa na Maidana hii leo.
Ukiachilia mbali na Justin Bieber, Kruu nzima ya Maywheather
inayofahamika kwa jina la ‘The Money Team’ itakuwepo uwanjani hapo kwa
ajili ya kumpa kampani bondia huyo anayeshikilia mataji makubwa
mbalimbali ya mchezo wa ngumi Duniani.
Taarifa zinasema kwamba mpambano huo utamfanya Maywheather
aweke kibindoni kiasi cha dola za kimarekani milioni 32(Tsh Bilioni 51)
wakati mpinzani wake akiondoka na kitita cha dola milioni 1.5(Tsh
bilioni3 ).
Hii sio mara ya kwanza kwa Justin Bieber kumsindikiza bondia
huyo, kwani imekuwa ni kama desturi kwa baadhi ya wasanii nyota
kumsindikiza mkali wao huyo, miongoni wao ni pamoja na Lil Wayne, 50
cent na familia ya YMCMB kwa ujumla.
Bondia
Marcos maidana(Wa kwanza kulia) na Floyd Money maywheather (Wa kwanza
Kushoto) wakipima uzito kwa ajili ya mpambano wa hii leo.
JUSTIN BIEBER KUMSINDIKIZA BONDIA FLOYD ‘MONEY’ MAYWHEATHER KATIKA PAMBANO LAKE LA LEO DHIDI YA MAIDANA
Reviewed by crispaseve
on
01:53
Rating:


Post a Comment