KATIBU MKUU WA CCM,KINANA ATEMBELEA WANANCHI WAISHIO KANDO KANDO YA BANDARI YA KASANGA,WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na baadhi ya viongozi wa chama
Wilaya ya Kalambo,wakikatiza kwenye Ofisi ya CHADEMA,ambayo inadaiwa
imefungwa miaka mitatu 3 sasa kwa kushindwa kulipia pango.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka mchanga kwenye mashine ya kufyatulia
tofali ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa jengo la CCM,wilayani Kalambo
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akibeba tofali aliyoifyatua,ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa jengo la CCM,wilayani Kalambo
Wajumbe wakifurahia jambo mara baada ya Ndugu Kinana kuzungumza jambo mbele yao.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe nyumbani kwa Mjumbe wa
shina No.1,Bwa.Apolinali Kwidikwa,katika kata ya Kateka,wilayani Kalambo
mkoani Rukwa mapema jana jioni.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha
Matai,katika wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa mapema jana jioni.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kijiji
cha Kasanga Wilayani Kalambo jana jioni,kabla ya kufanya mkutano wa
hadhara na kuzunguma na wananchi hao mambo mbalimbali ikiwemo
Afya,maji,Elimu.Barabara na mengineyo.
Baadhi ya Wanachi wa kijiji cha Kasanga wilayani Kalambo wakifuatilia mkutano.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa,Balozi Ally Karume akihutubia mbele ya
wananchi wa kijiji cha Kasanga,Wilayani Kalambo mkoani Rukwa mapema
jana,wakati wa mkutano wa hadhara.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akila kiapo na Sehemu ya Wanachama wapya
waliojiunga na CCM na kukabidhiwa kadi,ambapo Wanachama wapya 266
wamejiunga na chama hicho katika kata ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani
Rukwa.
Sehemu
ya Wanachama wapya waliojiunga na CCM na kukabidhiwa kadi na Ndugu
Kinana wakila kiapo.Wanachama wapya 266 wamejiunga na chama hicho katika
kata ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizawadiwa zawadi kutoka kwa akina mama wa
kata ya Kasanga,iliopo ndani ya wilaya mpya ya Kalambo,mkoani Rukwa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Kasanga,iliopo
ndani ya wilaya mpya ya Kalambo,mkoani Rukwa mapema jana jioni.Kinana
bado yupo Mkoani Rukwa na ziara yake ya kuimarisha chama,kukagua miradi
mbalimbali,ikiwemo na kusikiliza kero za wananchi.
Baadhi
ya akina mama wakazi wa kata ya Kasanga wilayani kalambo wakishangilia
jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akizungumzia
mambo mbalimbali ikiwemo utatuzi wa masuala ya Afya,Elimu,Barabara na
maji.
Waendesha
bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuelekea
kijiji cha Matai,Makao makuu ya Wilaya ya Kalambo kuendelea na ziara
yake ya kuimarisha chama,kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata taarifa ya hali ya kisiasa katika wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa mapema jana.
KATIBU MKUU WA CCM,KINANA ATEMBELEA WANANCHI WAISHIO KANDO KANDO YA BANDARI YA KASANGA,WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA
Reviewed by crispaseve
on
06:36
Rating:

Post a Comment