Header AD

KINANA ATEMBELEA WANANCHI PEMBEZONI MWA WILAYA YA NKASI, AKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA UBOVU WA BARABARA



Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwafurahia vijana aliowakuta wakifanya kazi katika kijiji cha Wampembe kilichopo kilometa 100 kutoka mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi. Vijana hao wanafanyakazi katika sekta ya afya na ujenzi.Pichani kulia ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka,Injinia wa maji wilaya ya Nkasi,Bwa.Simon Sadala,Fundi Mkuu Ujenzi,Bwa.Athanael Rwamlema na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nkasi,Bwa.Kimulika Galikunga.
Ndugu Kinana akikagua ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Wampembe wilayani Nkasi mkoani Rukwa akipata maalezo mafupi kuhusiana na ujenzi wa kituo hicho cha afya kuyoka kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka.Kituo hicho kimejengwa kwa msaada mkubwa wa Africare kwa kushirikiana na Plan International,ambacho ni maalum kwa ajili ya afya mama na watoto na upasuaji
Sehemu ya jengo la kituo cha Afya kikiendelea na ujenzi katika kijiji cha Mwampembe,wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano huo.
Pichani Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Wampembe, jana,Aprili Mosi, 2014. Na zinazoendelea ni picha zaidi za ziara hiyo na changamoto hizo alizokumbana nazo kama zilizvyopigwa na Bashir Nkoromo aliyeko kwenye ziara hiyo. 

Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Abdulrahman Kinana jana, aliendelea na ziara yake katika mkoa wa Rukwa, kwa kutembelea wananchi walioko pembezoni mwa mkoa huo, ambapo alifika hadi katika Kata ya Wampembe iliyopo zaidi ya kilometa 100 kutoka mji mdogo wa Namanyere wilaya ya Nkasi iliyomo kata hiyo.

 Katika safari iliyomchukua zaidi ya saa tisa, Kinana na msafara wake alikumbana na changamoto kubwa ya ubovu wa barabara kutoka Namanyere hadi kwenye vijiji vya kata hiyo kutona na magari kunasa mara kwa mara kwenye tope na makorongo,kwa kuwa barabara haijapata kufanyiwa matengenezo kwa muda mrefu.

 Kufuatia kujionea changamoto hiyo, Kinana amewambia wananchi wa vijiji vya Wampembe na Ntemba, kuwa ataishauri serikali kuifanya barabara hiyo iwe chini ya Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) badala ya sasa ambapo ipo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi na hivyo kuwa vigumu kupatikana fedha za kutosha kujenga barabara hiyo. 
Kinana akizungumza na wananchi saa mbili usiku, baada ya kuzuia msafara wake eneo la  kijiji cha Ntemba kaya ya Kate akitoka Kata ya Wampemba kwenda Sumbawanga mjini.
KINANA ATEMBELEA WANANCHI PEMBEZONI MWA WILAYA YA NKASI, AKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA UBOVU WA BARABARA  KINANA ATEMBELEA WANANCHI PEMBEZONI MWA WILAYA YA NKASI, AKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA UBOVU WA BARABARA Reviewed by crispaseve on 08:02 Rating: 5

No comments

Post AD