WAKAZI WA SUMBAWANGA VIJIJIJINI WAVUTIWA NA UTENDAJI KAZI WA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA.!
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya Waalimu wa shule ya
sekondari Ilemba,Sumbawanga Vijijini,alipokwenda kukagua ujenzi wa bweni
la wasichana wa shule hiyo,iliopo nje ya kilometa 104 kutoka Sumbawanga
Mjini.
Sehemu ya bweni hilo la Wasichana,ujenzi wake ukiendelea.
Ndugu
Kinana akipokea taarifa ya Shule ya Sekondari ya Ilemba kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Sumbawanga Vijijini,Bwa.Abeid
Missana.Shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 237 inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya
Sayansi,Nyumba za walimu na idadi ya waalimu waliopo.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo hilo la Bweni la wasichana shule ya sekondari ya Ilemba.
Katibu
Mkuu wa CCM,akiwa ameongozana na baadhi ya Viongozi wa Chama Wilaya na
Mkoa wakielekea kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa
Kituo cha Afya,kilichopo kata ya Ilemba;Sumbawanga Vijijini
Kinana akipitishwa kukagua ujenzi wa zahanati hiyo na Ofisa Mtendaji wa Kijiji,Kata ya Ilemba,Bwa.Desdei Kayola (pichani kati)
Muonekano
wa ujenzi wa kituo hicho cha afya,kata ya Ilemba ambacho kikikamilika
kitaokoa maisha ya idadi kubwa ya watu,ambayo inapotea kutokana na uduni
wa huduma ya afya iliyopo sasa,hivyo kituo hicho kitatatua changamoto
zilizopo za huduma ya afya.
Kinana akikagua ujenzi wa kituo cha Polisi kata Ilemba,Sumbawanga vijijini.
Kinana akishiriki
ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Ilemba, Sumbawanga Vijijini. Ameahidi
kutoa mifuko 50 ya saruji na bati 50 kumalizia ujenzi wa kituo hicho
Wananchi wa kata ya Ilemba wakiwa na mabango Wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Kinana
Wananchi
wa Kijiji cha Ilemba wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Ilemba.
Baadhi
ya Wanachama wapya wapato 300 kutoka kata ya Ilemba, waliojiunga na
chama cha CCM,wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi za chama hicho
na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi, katika kijiji cha Ilemba,
kata ya Ilemba, alipohutubia wananchi katika kata hiyo akiwa katika ziara
ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana
nao njia za kuzitatua katika wilaya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa.
Wananchi
wa kijiji cha Ilango,Kata ya Ilemba,Sumbawanga vijijini wakimpokea
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa aina yake alipokuwa akiwasili
kijijini hapo ambapo pia aliongea na kuwasikiliza matatizo yao ikiwemo
na kuyafanyia kazi.
WAKAZI WA SUMBAWANGA VIJIJIJINI WAVUTIWA NA UTENDAJI KAZI WA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA.!
Reviewed by crispaseve
on
09:33
Rating:

Post a Comment