Header AD

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA SIKU NANE MKOANI SINGIDA



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi za CCM kata ya Ighombwe ambapo aliwahimiza viongozi wa CCM kujenga ofisi zenye uwezo wa kutoa  msaada wa kijamii ikiwa pamoja na elimu za ujasiliamali .
 Baadhi ya wakazi wa kata ya Ighombwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Ighombwe na kuwataka kudumisha moyo wa mshikamano katika kuleta maendeleo ya pamoja.
 wakazi wa kata ya Ighombwe wakila kiapo baada ya baadhi yao kujiunga na chama hicho cha ccm.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (haoenekani pichani) akizungumza na Wananchi baada ya kushiriki ujenzi wa Zahanati,kata ya Sepuka wilayani Ikungi 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Sepuka Wilayani Ikungi,jimbo la Singida Magharibi,na kuwataka kuungana katika kushiriki kuleta maendeleo hasa yale yanayohusu jamii kama kujenga shule, maabara na zahanati.
 Mkutano wa hadhara uliondaliwa na CCM,ukiendelea katika viwanja vya shule ya sekondari Sepuka,wilayani Ikungi,Singida Magharibi .
 Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana (haonekani vizuri pichani) akizindua shina la Vijana wa Boda Boda katika kata ya Puma,wilayani IKungi mkoani Tabora.
  Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua shina la Kina Mama wa UWT,ambao hujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiliamali ikiwemo na Ushonaji wakiwa katika kikundi cha Ebeneza,Puma,wilayani IKungi mkoani Tabora.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki kuvuna viazi vitamu pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai kwenye shamba la mkulima Bernardo Razalo
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA SIKU NANE MKOANI SINGIDA  KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA SIKU NANE MKOANI SINGIDA Reviewed by crispaseve on 01:02 Rating: 5

No comments

Post AD