KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI TABORA,ALA CHAKULA CHA MAMALISHE KUWAUNGA MKONO,AHITIMISHA ZIARA YAKE KWA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA/
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
katika Uwanja wa Stendi Kuu ya Zamani mjini Tabora, baada ya kumaliza
ziara yake ya siku 11 katika mkoa huo, ya kuimarisha uhai wa chama,
kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa
kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
Wakazi
wa Mji wa Tabora Mjini wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa
hadhara uliondaliwa na CCM leo jioni,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana amehitimisha siku za ziara yake ya siku 11 mkoani humo,ya ya
kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya
maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi
ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi
na kuzitafutia ufumbuzi.Kinana na msafara wake kwesho wataelekea mkoani
Singida kwa ziara siku kadhaaa tena.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa
hadhara wa CCM, Mjini Tabora leo, ambapo aliwafananisha Wapinzani na
Boko Haramu wa waasi wa Nigeria kwa kuwachonganisha wananchi kwa
maneno,hali ambayo imeeleza kuwa kinaweza kusababisha vurugu nchini.
Katibu
Mkuu wa CC,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa
halmashauri kuu ya CCM,Wilaya ya Tabora mjini mapema leo kabla ya kwenda
kwenye mkutano wa hadhara,aidha Kinana katka ziara yake wilayani Tabora
alikagua miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa umwagiliaji,kuweka jiwe la
msingi katika ofisi za CCM,kukagua mradii wa ujenzi wa
hospitali,kuzindua mradi wa matofali wa akina mama na mengineyo mengi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na Wazee waasisi wa chama cha TANU mjini Tabora leo.
Kinana akinawishwa na Mamalishe kabla ya kupakuliwa msosi wa nguvu.
Kinana
akihudumiwa na Mama Lishe alipokwenda kula yeye na msafara wake kwa
akina mama lishe eneo la Stendi Mpya Tabora mjini. Kushoto ni Mbunge wa
Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tabora, Aden Rage ukiungana na Kinana kula msosi kwa mamaLishe mjini Tabora leo.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Mkuu wa Mkoa wa Tabora,
Fatma Mwassa wakipata mlo kwa Mama Lishe mjini Tabora leo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiapata mlo wa mchana kwa Mama ntilie katika
stendi mpya ya mabasi mjini Tabora,Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Tabora
Mjini ,Mh Aden Rage,katikati ni Mbunge wa viti maalum CCM mkoani
Tabora,Mh.Munde Tambwe wakishiriki pamoja na naye katika mlo huo
sambamba na vijana wa mjini Tabora.
Naibu
Waziri wa Maji,Mh.Amoss Makala akitoa ufafanuzi kwa wakazi wa Tabora
mjini kuhusiana na suala zima la upatikanaji maji na mikakayi yake
katika mkoa huo,ambapo imeelezwa kuwa mkoa huo una tatizo kubwa la maji
Baadhi
ya Wabunge mbalimbali walioshiriki kwenye mkutano huo wa Hadhara
uliofanyika mjini Tabora,ikiwa ni siku ya mwisho ya kuhitimisha ziara ya
siku 11 ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mkoani humo.
Mbunge
wa jimbo la Mtera,Mh.Livingstone Lusinde akiwahutubia wakazi wa mji wa
Tabora mjini leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na chama
cha CCM.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais,Mh. Ummy
Mwalim akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuuponda Ukawa kwa
kitendo chake cha kutoka bungeni kwa sababu zisizoeleweka wakati wa
Bunge la Katiba,Mh.Ummy pia aliwatia shime akina mama kuwa na mshikamano
katika suala zima la kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali
walizomo,na kuacha kubweteka wakisubiri waletewe maendeleo.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa akihutubia katika mkutano wa hadhara wa
CCM, ambapo alimpongeza Katibu Mkuu Kinana kwa kufanikisha ziara yake
mkoani humo na kumaliza salama.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Umma), Steven Wassira akihutubia
katika mkutano wa hadhara na kuwaponda viongozi wa Ukawa wa kususia
mkutano wa Bunge la Katiba bila kuwa na sababu za msingi.
KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI TABORA,ALA CHAKULA CHA MAMALISHE KUWAUNGA MKONO,AHITIMISHA ZIARA YAKE KWA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA/
Reviewed by crispaseve
on
07:06
Rating:
Post a Comment