KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASILI WILAYA YA KALIUA,AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
Katibu
MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM,Wilaya ya Kaliua,katika ukumbi wa Millenium
mkoani Tabora mara baada ya kupokea taarifa mbalimbali za maendeleo ya
miradi na hali ya kisiasa wilayani Kaliua. Kinana yupo mkoani Tabora kwa
ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo
inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia
ufumbuzi.
Baadhi
ya Wananchi wa kijiji cha Usindi wakishuhudia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Zahanati ambayo tayari
imwekwishakamilika,isipokuwa inasubiri kibali na kukamilika nyumba ya
mganga.Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi
Nape Nnauye,ambapo walipokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo
Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya
Mkuu
wa CCM,Ndugu Kinana akipata taarifa fupi juu ya mradi wa ujenzi wa jengo
la nyumba ya Mganga wilayani Kaliua katika kijiji cha Usindi,Kata ya
Ushokora,Katika ziara hiyo ya siku 11,Kinana ameambatana na Katibu wa
NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye,ambapo walipokelewa na Mbunge
wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya .
Katibu
Mkuu wa CCM,dugu Kinana akilakiwa na Mbunge wa jimbo la Urambo
Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya,mara baada ya kuwasili wilayani
Kaliua,katika kijiji cha Usindi kata ya Ushokora akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye (hayupo pichani). mkoani Tabora.
Mbunge
jimbo la Urambo Mashariki,Mh.Samwel Sitta akisalimiana na Mbunge wa
jimbo la Urambo Magharibi Prof.Juma Kapuya mapema leo kwenye wilaya ya
Kaliua,mara baada uusindikiza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
aliyekuwa Wilayani Urambo Mashariki kwa ziara ya siku 11 ndani ya mkoa
wa Tabora.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa katika kijiji cha Usindi,Kata ya
Ushokora wilayani Kaliua mkoani Tabora mapema leo asubuhi,akiwa
ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye na
kupokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya
Ndugu
Kinana pichani na viongozi wengine wa CCM,wakienda kukagua Mradi wa
ujenzi wa Zahanati na nyumba ya Mganga,katika kijiji cha Usindi kata ya
Ushokora wilayani Kaliua mkoani Tabora.
Ndugu Kinana wat tatu kulia akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la
Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya,kulia ni Katibu wa NEC
Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye na viongozi wengine wa
CCM,wakitoka kukagua Mradi wa ujenzi wa Zahanati na nyumba ya
Mganga,katika kijiji cha Usindi kata ya Usindi wilayani Kaliua mkoani
Tabora.
KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASILI WILAYA YA KALIUA,AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
Reviewed by crispaseve
on
07:37
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
07:37
Rating:









Post a Comment