Header AD

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA IABADA MAALUM YA KUSIMIKWA ASKOFU MTEULE ALEN SISO WA KANISA LA METHODIST TANZANIA- JIMBO TEULE LA MASHARIKI NA PWANI, DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, baada ya kumkabidhi Katiba na Kanuni za Kanisa la Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya Kuwekwa Wakfu (kusimikwa) askofu huyo, iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli dhehebu la Methodox, Jimbo teule la Pwani na Mashariki lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia Waumini wa dini ya Kikristo wa Kanisa la Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya Kusimikwa Askofu Mteule Alen Legeza Siso, iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli, Jimbo teule la Pwani na Mashariki lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Methidist Tanzania, Dkt. Mathew Byamungu, baada ya Ibada maalum ya kusimikwa Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, (kulia) kuwa Askofu wa Jimbo la Mashariki na Pwani iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli, Jimbo hilo lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Methidist Tanzania, Mathew Byamungu, akimsimika Askofu Alen Legeza Siso, kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mashariki na Pwani, Makanisa ya Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya kuwekwa Wakfu Askofu huyo iliyofanyika leo Mei 3, 2014, kwenye Kanisa la Emanueli lililopo Bunju jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na baadhi ya wachungaji wa Kanisa la Emanueli, Jimbo la Mashariki na Pwani, wakati alipowasili jimboni hapo kwa ajili ya kuhudhuria Ibada maalum ya Kusimikwa, Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014.
 Baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo waliohudhuria Ibada hiyo maalum ya kumsimika Askofu Mteule, Alen Siso
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA IABADA MAALUM YA KUSIMIKWA ASKOFU MTEULE ALEN SISO WA KANISA LA METHODIST TANZANIA- JIMBO TEULE LA MASHARIKI NA PWANI, DAR ES SALAAM  MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA IABADA MAALUM YA KUSIMIKWA ASKOFU MTEULE ALEN SISO WA KANISA LA METHODIST TANZANIA- JIMBO TEULE LA MASHARIKI NA PWANI, DAR ES SALAAM Reviewed by crispaseve on 16:24 Rating: 5

No comments

Post AD