MAMA TUNU PINDA AOMBA WATU NA MASHIRIKA MBALIMBALI KUSAIDIA KUCHANGIA KATIKA KUENDELEZA ELIMU KWA WATOTO NA VIJANA WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALIBINO)
Mlezi
wa chama cha wake wa viongozi Mama Tunu Pinda akipokea vitabu vyenye
thamani ya shilngi milioni 35 kutoka kwa Meneja Mkuu wa kituo cha
kuendeleza vipaji kwa vijana THT Bwana Mwita Mwaikenda na anaye shuhudia
ni Mwenyekiti wa chama cha wake wa viongozi Germina Lukuvi msaada huo
wa vitabu ni kwaajili ya kusaidia Elimu kwa watoto na vijana wenye
ulemavu wa ngozi (ALIBINO) sherehe hiyo ya makabidhiano imefanyika
katika makazi ya waziri mkuu jijini Dar es salaam.
picha ya pamoja
Mlezi wa chama cha wake wa viongozi Mama Tunu Pinda (pichani kati) akizungumza na Wanahabari kabla ya ya kupokea vitabu vyenye thamani ya shilngi milioni 35 kutoka kwa Meneja Mkuu wa kituo cha kuendeleza vipaji kwa vijana THT Bwana Mwita Mwaikenda (pichani kulia) na kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha wake wa viongozi Germina Lukuvi ..
Mlezi wa chama cha wake wa viongozi Mama Tunu Pinda (pichani kati) akizungumza na Wanahabari kabla ya ya kupokea vitabu vyenye thamani ya shilngi milioni 35 kutoka kwa Meneja Mkuu wa kituo cha kuendeleza vipaji kwa vijana THT Bwana Mwita Mwaikenda (pichani kulia) na kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha wake wa viongozi Germina Lukuvi ..
THT
yatoa vitabu kwa maktaba ya walemavu wa ngozi Kanda ya Ziwa
Nyumba ya vipaji Tanzania (THT) imetoa
vitabu vya Sayansi, Sanaa na Hesabu kwa maktaba ya walemavu wa ngozi
inayotarajiwa kujengwa na taasisi isiyo ya Kiserikali ya New Millennium Group.
Vitabu hivyo vyenye thamani ya jumla ya
shilingi milioni 35 vimetolewa kwa lengo la kusaidia kukuza elimu Tanzania hasa
kwa jamii ya walemavu wa ngozi, ikiwa ni mchango wa THT kwa huduma za jamii.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,
Meneja Mkuu wa Nyumba ya Vipaji Tanzania, Mwita Mwaikenda alisema taasisi yake
iliona changamoto ya vitabu baada ya taasisi ya New Millennium Group kutembelea
vituo vya maalbino vya kanda ya ziwa mwanzoni mwa mwaka huu.
‘Msaada huu wa vitabu sisi kama THT
tumeutoa ili kuiwezesha maktaba ya walemavu kupata vitabu vya kujisomea na
hivyo kujiongezea maarifa baina yao’ alisema Mwita. Kwa upande wake Mlezi wa Taasisi ya New
Millenium Group, Mama Tunu Pinda, alisema wanaishukuru THT kwa msaada huo ambao
alisema ni muhimu sana kwa ajili ya lengo lao la kusaidia kuiwezesha kielimu
jamii ya watoto wenye ulemavu wa ngozi.
‘Hakika msaada huu utasaidia kwa kiasi
kikubwa katika kufanikisha lengo la kuanzisha maktaba kwa watoto wenye ulemavu
wa ngozi, na tunaaamini msaada huu utawapa changamoto wadau wengine kusaidia
kukamilisha maktaba hii ya kwanza kabisa kuhudumia watu wenye ulemavu wa ngozi’
alisema Mama Pinda.
Naye Mwenyekiti wa New Millennium Group,
Mama Germina Lukuvi anasema pamoja na vituo hivyo kuwa na sehemu ya malazi kwa
maalbino bado kumekuwa na changamoto ya sehemu za kujisomea na New Millennium
Group itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha changamoto hizo
zinatatuliwa.
MAMA TUNU PINDA AOMBA WATU NA MASHIRIKA MBALIMBALI KUSAIDIA KUCHANGIA KATIKA KUENDELEZA ELIMU KWA WATOTO NA VIJANA WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALIBINO)
Reviewed by crispaseve
on
00:05
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
00:05
Rating:



Post a Comment