MAN CITY YANUSA UBINGWA WA EPL, YAIGONGA BAO 4 – 0 ASTON VILLA
Manchester
City imeonyesha nia ya dhati kabisa ya kutaka kutwaa ubingwa wa ligi
kuu ya England ‘EPL’ baada ya kuipa kipigo cha mabao 4 kwa nunge klabu
ya Aston Villa katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Etihad hapo jana
Mabao mawili ya mwanzo ya City yalifungwa na Dzeko, Stevan Jovetic aliyefunga goli la tatu kabla ya kiungo tegemezi wa timu hiyo ‘Yaya Toure’ kupachika bao la nne mnamo dakika ya 90 na kuiwezesha timu yake kuibuka kidedea kwa ushindi huo mnono.

Wachezaji wa City wakishangilia baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa.
Ushindi walioupata City umewaweka kilele mwa ligi hiyo
kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya Liverpool ambayo kwa sasa
inakamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 81 huku ikiwa imebakisha mchezo
mmoja mkononi.Kwa upande wa Liverpool yenyewe bado inakibarua kigumu hasa baada ya matokeo ya ushindi waliyoyapata City dhidi ya Aston Villa. Majogoo hao wa jiji la London watavaana na Newcastle jumapili ijayo.
Tazama Video za magoli hapo chini
MAN CITY YANUSA UBINGWA WA EPL, YAIGONGA BAO 4 – 0 ASTON VILLA
Reviewed by crispaseve
on
06:46
Rating:



Post a Comment