MASHINDANO YA DATS YAZINDULIWA MKOANI MOROGORO, MIKOA TISA KUSHIRIKI
Mwenyekiti
wa chama cha Dats Tanzania Gesase Waigama akiongea wakati wa ufunguzi
wa mashindano ya mchazo huo unaoshirikisha mikoa ya Dar es Salaam,
Dodoma, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Kagera, Arusha na wenyeji wao
Morogogoro ambapo katika mashindano hayo yaliodhaminiwa na bia aina ya
Safari mshindi wa kwanza atatoka na kitita cha shilingi 600,000 hapo
kesho.
Baadhi
ya washiriki wa mchezo huo wakifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa
shindano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Magunila Kihonda Mjini
Morogoro.
Wahsiriki wa shindano hilo kutoka mikoa mbailimbali wakiwa katika ukumbi huo wakishuhudia pambano hilo.
Irene Kihupi mchezaji kutoka mkoa wa Dar es Salaam akiwa katika pambano hilo.
Joyce Laize mchezaji kutoka mkoa wa Arusha akiwa katika pambano hilo.
Mwenyekiti huyo wa Dats akizindua mchezo huo ili kuruhusu pambano kuanza rasmi.
Baadhi ya wachezaji wakiwa katika pambano hilo
Frolida Namajojo katibu wa Dats mkoa wa Morogoro akiwa katika mazoezi kabla ya kuanza mchezo huo.
WANACHAMA
wa chama cha Darts Taifa (TADA) wameyaomba makampuni yanayodhamini
michezo mbali mbli nchini kuwekeza kwenye chama hicho ili kuweza kukuza
uchumi,michezo pamoja na kuongeza pato la taifa.
Wanachama hao waliyasema hayo Mei 24 mwaka huu kwa nyakati tofauti watika wa mashindano ya mabingwa wa chama hicho yanayofanyika mkoani hapa.
Walisema
kuwa mchezo huo ni mzuri lakini unachangamoto ya gharama ambapo alisema
kuwa mara zote yanapoandaliwa mashindano hayo kila mwanachama anatakiwa
kujitegemea mwenyewe.
Aidha
waliwaomba kopa Coca Cola kuandaa utaratibu wa kupeleka mchezo huo
mashuleni ili kuweza kuibua vipaji vya mchezo huo kuanzia ngazi ya
shule.
Kwa
upande wake katibu mkuu wa chama hicho Kale Mwigonja alisema kuwa
shindano hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Safari Lager
linalenga kunua mchezo huoikiwa I pamoja na kujiandaa na Afrika
Mashariki linalotarajia kufanyika mwezi juni mwaka huu Mkoani Dodoma.
Alisema
kuwa mashindano hayo yanashirikisha virabu 32 kutoka katika mikoa mbali
mbali nchni ambapo alisema kuwa washindi watapata zawadi mbalimbali
ikiwemo ikombe pamoja na zawadi za pesa taslimu ambapo alisema kuwa
mshindi wa kwanza atapata sh.laki 6 na kikombe ,wa pili laki 4 na
kikombe na watatu laki 3.
MASHINDANO YA DATS YAZINDULIWA MKOANI MOROGORO, MIKOA TISA KUSHIRIKI
Reviewed by crispaseve
on
14:46
Rating:
Post a Comment