MBUNGE NA DIWANI CHADEMA WALALAMIKIWA NA WANANCHI KUKWAMISHA MAENDELEO YA JIMBO KWA MIAKA MINNE
ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi ukiendelea katika Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu,ambaye anadaiwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo.
Mmoja
wa Viongozi wa CCM,Wilaya akimpatia tofari Kinana walipokuwa wakisaidia
ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi, katika Jimbo la Singida Mashariki
la Mbunge Tundu Lissu. Mbunge huyo anadaiwa kuwakataza wananchi
kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo.
Lakini baada ya kuona watoto wao wanateseka kwa kukosa elimu wananchi
wameamua kupuuza katazo hilo na kuanza kujitolea kujenga vyumba hivyo
vya madarasa.
Jengo
la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata
hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya
Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu
Lissu kudaiwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba
ya madaktari.
Kinana akizungumza na baadhi ya wananchi nje ya engo
la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata
hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya
Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu
Lissu kuaiwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba ya
madaktari.
Kinana akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi, Unyaghumpi
Wanafunzi
wa elimu ya awali, wakifundishwa na mwalimu Juliana Joseph huku wakiwa
wamekaa sakafuni na juu ya paa kukiwa wazi katika moja ya vyumba vya
madarasa ya Shule ya Msingi, Unyaghumpi vilivyozuiliwa kujengwa na
Mbunge Tundu Lissu kwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha na kuwaambia
kuwa fedha zote zitatoka serikalini.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaidia kuvuna mtama na uwele kwenye
shamba bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi katika Kata ya
Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida,wakati wa ziara
yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi
wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya
CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza
kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika
Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge Tundu Lissu wa Chadema, Kinana
alishuhudia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ujenzi wake
umekwamishwa na mbunge huyo kwa kuwzuia wananchi kuchangia fedha za
miradi hiyo akidai kuwa fedha zote zitatoka serikalini.
Baadhi
ya miradi iliyosimama aliyoikagua Kinana, ni Zahanati ya Kimbwi ukiwemo
ujenzi wa nyumba za waganga ambayo imeishia kwa kupigwa msingi wa zege.
Vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Unyaghumpi ambapo walikutwa
watoto wa shule ya awali wakifundishwa huku wakiwa wamekaa sakafuni na
juu kukiwa wazi bila kuzekwa. Miradi mingine iliyokwama ni ujenzi wa barabara, mawasiliano ya simu, maji na umeme
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi anayemiliki shamba la mtama na uwele,ambalo Kinana alishiriki kuvuna,katika Kata ya Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
ulofanyika katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la
Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza
wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo
kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala
ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala UKAWA na kutukana
matuzi bungeni.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
ulofanyika katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la
Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza
wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo
kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala
ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala ya UKAWA na
kutukana matusi bungeni.
Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi.
Aliyekuwa
kiongozi wa Chadema, Ismail Gwau, akikabidhi vifaa vya ofisi yake kwa
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Nape na hatimaye kujiunga chama cha
CCM, katika Mkutano huo wa hadhara.
Aliyekuwa
kiongozi wa Chadema, Ismail Gwau, akitupilia mbali bendera ya CHADEMA
mara baada ya kutangaza kujiunga na chama cha CCM,katika Mkutano huo wa
hadhara.
Sehemu ya Wakazi wa Ikungi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara.
Kinana akioneshwa bwawa la kukusanyia maji ambayo hutumika kumwagilia mashambani kwa njia ya matone.
Wafanyakazi wa wakichuma maharage katika shamba hilo.
Kinana
akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Singida
Agriculture, Ally Mohamed jinsi wanavyomwagilia mashamba yao kwa
kutumia njia ya matone kwenye shamba la kumwagilia lenye ukubwa wa ekali
200 katika Kijiji cha Mkiwa, wilayani Ikungi, Singida.
Kinana
akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Singida
Agriculture, Ally Mohamed jinsi wanavyozalisha maharage kwenye shamba
la kumwagilia lenye ukubwa wa ekali 200 katika Kijiji cha Mkiwa,
wilayani Ikungi, Singida.
Baadhi
ya wafanyakazi wa shamba hilo wakiwa wamebeba ndoo zenye maharage hayo
tayari kuyapeleka kwenda kufungasha kwenye makasha tayari kusafirishwa
kwenda kuuzwa nje ya nchi.
maharage yakifungashwa kwa ajili ya maandalizi ya kuuzwa nje ya nchi
Kinana
akisaidia kufungasha maharage hayo, kwa ajili ya maandalizi ya kuuza
nje ya nchi.Kulia ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Singida, Mgana Msindai
pamoja na Nape Nnauye pichani kati.
MBUNGE NA DIWANI CHADEMA WALALAMIKIWA NA WANANCHI KUKWAMISHA MAENDELEO YA JIMBO KWA MIAKA MINNE
Reviewed by crispaseve
on
01:30
Rating:
Post a Comment