MKONGWE RIO FERDINAND AMPIGIA PANDE VAN GAAL MAN UNITED, ASEMA JAMAA ANAFAA KINOMA!

BEKI
mkongwe wa Manchester United, Rio Ferdinand anaamini Louis van Gaal ni
mtu sahihi kukabidhiwa majukumu ya ukocha mkuu klabuni hapo.
Kutangazwa
kwa Mholanzi huyo kama mirthi wa David Moyes kulistishwa jana alhamisi
ili kumuacha huru wakati huu akiiandaa timu ya taifa ya Uholanzi kucheza
mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador.
Van
Gaal amewahi kuongeza klabu kubwa za dunia, hivyo beki huyo wa kati
ambaye hatakuwepo Old Trafford msimu ujao baada ya kutangaza kuondoka
majira ya kiangazi mwaka huu amesema kocha huyo anaweza kuleta mafanikio
katika michuano ya ligi kuu.
“Anaonekana
mtu imara sana na muelekezaji. Ana uelewa na ufahamu mkubwa kwa kila
anachotaka kufanya. Unatakiwa kuwa hivyo katika klabu kama Man United,”
Ferdinand aliwaambia waandishi wa habari.
MKONGWE RIO FERDINAND AMPIGIA PANDE VAN GAAL MAN UNITED, ASEMA JAMAA ANAFAA KINOMA!
Reviewed by crispaseve
on
02:37
Rating:

Post a Comment