MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AKAGUA UJENZI WA MIRADI YA MAJI KATIKA MANISPAA YA SUMBAWANGA, APIGA MARUFUKU UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (Mb) katikati akitoa maelekezo kwa
watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Mkandarasi
anaejenga mradi wa maji wa kijiji cha Malonje ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa ahadi za Serikali za kufikisha huduma muhimu kwa
wananchi. Mradi huo wa maji ambao unaelekea kukamilika umefadhiliwa na
benki ya dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa gharama ya
Tsh. Milioni 279. Katika maagizo aliyoyatoa ni pamoja na kupiga marufuku
shughuli zote za kilimo na ufugaji karibu na vyanzo vya maji kulinda
vyanzo hivyo.
Sehemu
ya banio la kukingia maji kwenye chanzo cha maji (chemchem) katika
kijiji cha Malonje ambalo ni sehemu ya mradi huo, baadhi ya wananchi
wameonekana kuendesha shughuli zao za kilimo na ufugaji karibu na chanzo
hicho ambapo wamepigwa marufuku kuendeleza shughuli hizo za uharibifu
wa chanzo hicho cha maji.
Bwana
Danford Anania Kaimu Injinia wa Maji Manispaa ya Sumbawanga wa pili
kulia akitoa maelezo ya tenki la maji lenye ujazo wa lita 45, 000 kwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya. Tenki hilo limejengewa pampu
itakayotumia nguvu ya nishati ya jua kusukuma maji katika vijiji vya
jirani vya Malonje ikiwa ni sehemu ya mradi wa maji wa Kijiji cha
Malonje katika Manispaa ya Sumbawanga.
Banio
la kukinga maji kwenye chanzo (chemchem) ikiwa ni sehemu ya ujenzi wa
mradi wa Maji katika kijiji cha Mlanda Manispaa ya Sumbawanga ambapo
mradi huu utakaotumia zaidi ya Tsh. Milioni 394 unajengwa na mkandarasi
Safari General Traders na unategemewa kuhudumia wanachi wa kijiji cha
Mlanda. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya alitembelea jumla
ya miradi mitano ya Maji katika Manispaa ya Sumbawanga ambayo ni
Malonje, Mlanda, Pito, Chilenganya na Kanondo. Aliwataka wakandarasi
waharakishe kumaliza kazi walizobakisha ili wanancni waweze kupata
huduma hiyo muhimu ya maji. Aidha alikataa kukagua moja ya mradi kwa
vile mkandarasi husika amekua akitoa visingizio mbalimbali vya
kutokumaliza kazi.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Malonje muda mfupi baada ya kukagua mradi wa maji na Zahanati katika
kijiji hicho, aliwataka wananchi hao kuwaendeleza watoto wao kielimu na
kushirikiana na uongozi wa kijiji katika kuhifadhi mazingira na kulinda
vyanzo vya maji. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawannga Ndugu
William Shimwela.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AKAGUA UJENZI WA MIRADI YA MAJI KATIKA MANISPAA YA SUMBAWANGA, APIGA MARUFUKU UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI
Reviewed by crispaseve
on
07:13
Rating:
Post a Comment