MO ATAKA MADHEBEBU YA DINI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KULETA MAENDELEO ENDELEVU
Mbunge
wa jimbo la Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na
waumini wa Msikiti wa kijiji cha Mtamaa wakati wa ziara yake ya siku
tatu jimbo kwake.
Na Nathaniel Limu, Singida
MBUNGE
wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Gulam Dewji amewahimiza waumini wa
madhahebu mbalimbali ya dini kuendelea kushirikiana na serikali ili
kurahisisha upatikanaji wa maendeleo endelevu.
Mbunge
Dewji maarufu kwa jina la MO,ametoa wito huo hivi karibuni kwa nyakati
tofauti wakati akikagua ujenzi wa misikiti na makanisa jimboni kwake.
Amesema
madhehebu ya dini mbalimbali yana mchango mkubwa sana katika kusukuma
gurudumu la maendeleo,kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa kwa ujumla.
Mbunge MO akijumuika na waumini wa Kanisa la FPCT kutoa burudani wakati wa ziara ya MO.
"Mchango
wa madhehebu ya dini unasaidia mno kuendeleza amani na utulivu kuanzia
ngazi ya kaya,kijiji hadi taifa.Amani na utulivu uliopo hivi sasa ndio
unaotusaidia tumwabudu Mungu kwa uhuru na pia kujiletea maendeleo bila
vikwazo",amesema.
Dewji
amesema ili kuonyesha imani yake kubwa kwa madhehebu ya dini safari hii
ameamua kukagua ujenzi wa makanisa na misikiti ya jimboni kwake ili
aweze kuyaunga mkono katika ujenzi huo unaoendelea.
"Ninyi
ni mashahidi wangu wazuri juu ya maendeleo ya sekta mbalimbali
tuliyoyapata jimboni mwetu kwa kushirikiana mimi na ninyi.Baada ya
kufanya makubwa kwenye sekta ya elimu,afya,barabara na maji,sasa
nimeamua kwa moyo wangu wote kuboresha ustawi wa madhehebu ya
dini",amesema.
Akifafanua
zaidi, amesema kupitia kwa katibu mkuu wa CCM taifa,anatarajia
kukabidhi misaada ya mabati na mifuko ya saruji yenye thamani ya zaidi
ya shilingi 127 milioni kwa misikiti 51 na makanisa 30.
MO ATAKA MADHEBEBU YA DINI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KULETA MAENDELEO ENDELEVU
Reviewed by crispaseve
on
02:42
Rating:
Post a Comment