MWENGE WA UHURU WAANZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA LEO
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka
kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi (kulia) Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe mapema leo,
baadae aliukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan
Kimanta ambapo umeanza mbio zake katika Wilaya hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisoma hotuba ya
mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Mkoani Rukwa ukitokea Mkoa
jirani wa Katavi mapema leo. Katika hotuba yake hiyo amesema Mwenge huo
utatembelea miradi ya maendeleo 28 na vikundi 27yote ikiwa na thamani ya zaidi
ya Tsh.bilioni nne (4). Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies
Pangisa.
Mke wa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akipiga picha na
Mwenge wa Uhuru mara baada ya Mwenge huo kuzindua nyumba ya makazi ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo mapema leo. Kushoto ni Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Bi Rachel Kassanda.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akiteta jambo na Katibu
Tawala wa Mkoa wa huo Ndugu Symthies Pangisa wakati wa mapokezi ya Mwenge wa
Uhuru Mkoani Rukwa leo ukitokea Katavi.
Ndugu Congores Kipozo Mwenyekiti wa Umoja wa Wafugaji wa Kijiji cha
Lunyala Wilayani Nkasi akiupigia saluti Mwenge wa Uhuru ulipotembelea Kijijini hapo
leo kuzindua mradi wa josho la mifugo.
Miongoni mwa Viongozi wa Mkoa wa Katavi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa
huo Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe watatu kulia mara baada ya kukabidhi mwenge wa
Uhuru kwa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa leo ambapo utakimbizwa katika Wilaya tatu na
Halmashauri nne za Mkoa huo kwa muda wa siku nne. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
MWENGE WA UHURU WAANZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA LEO
Reviewed by crispaseve
on
01:38
Rating:
Post a Comment