Baadhi
ya Viongozi Wakuu wa Afrika waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika ambao ulifunguliwa na Mh. Rais wa Rwanda
Paul Kagame. Mh. Kagame katika hotuba yake alisisitiza kuzijengea uwezo
sekta binafsi ili Afrika iweze kufikia uchumi wa kati kwa kipindi cha
miaka 50 ijayo. Aidha katika kufikia lengo hilo, Rais Kagame alisema
hatuna budi Afrika kuachana na migogoro na kutekeleza kwa vitendo
makubaliano yanayoafikiwa na Viongozi wa Afrika ili kujenga uchumi
imara kwa vizazi vijavyo.
Kikundi
cha Ngoma za asili cha Bollet Nationol–URUKEREREZA cha jijini Rwanda
kikitumbuiza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika unaofanyika Rwanda.
Mh.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Washiriki mbalimbali wa Mkutano wa
mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano
huo uliofunguliwa na Mh. Paul Kagame katika ukumbi wa Mount Karisimbi
Jijini Kigali Rwanda.
RAIS KAGAME AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MWAKA WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) UNAOFANYIKA JIJINI KIGALI RWANDA
Reviewed by crispaseve
on
22:55
Rating: 5
Post a Comment