Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) lampongeza Waziri Membe.
Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) linatoa pongezi za
dhati kwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
Mh. Bernard Membe kwa hatua na jitihada alizozifanya za kutafua na kufanikisha kambi ya mazoezi kwa Timu ya Taifa ya
ngumi inayojiandaa kushiriki mashindano
ya jumuiya ya madola yatakayofanyika July, 2014 Nchini Scotland.
Kwa hakika ni mmoja wa watanzania ambae ameguswa na
maandalizi ya Timu yetu ya Taifa kwa
kuitafatia kambi ya mazoezi ya kimataifa
Nchini Uturuki na Nchini China kwani timu yetu ilikuwa inafanya mazoezi katika
hali duni bila ya kuwa na vifaa vya
kisasa kulingana na mabadiliko ya mchezo wa ngumi duniani.
Kwa kufanya hivyo tunakuwa na uhakika mkubwa wa kupata
medali katika mashindano hayo ya Jumuiya ya Madola na Tanzania kutangazika vema
Kimataifa kupitia mchezo wa ngumi maana bado tunakumbuka historia nzuri ya ushiriki
waTanzania katika mashindano ya Jumuiya ya madola kwani kwa mara ya kwanza
Tanzania ilishiriki mwaka 1972 na Tanzania
kupata medali ya kwanza ya kimataifa baada ya Tanzania kupata uhuru, iliyoletwa na Bondia (LYTUS SIMBA) na
baada ya hapo baadhi ya mabondia walioleta medali ni kama wafuatao:
MICHAEL YOMBAYOMBA : (Dhahabu)
HAJI MATUMLA : (Fedha)
MAKOYE ISANGURA : (Shaba)
MWAMBEYA BAKARI
: (Shaba)
WILLY
ISSANGURA : (Shaba)
LUCAS MSOMBA : (Shaba)
Bado BFT tunamuomba azidi
kutusaidia vifaa zaidi hasa ulingo wa
kisasa na Computer inayotumika kuhesabia
point za ushindi wakati wa mashindano kwani Nchi zote duniani ndizo
wanazozitumia na niagizo kutoka chama cha ngumi cha dunia kwa wanachama wote
lazima waitumie katika mashindano..
Taarifa hii imeletwa kwenu na
Makore Mashaga
KATIBU MKUU.
Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) lampongeza Waziri Membe.
Reviewed by crispaseve
on
02:04
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
02:04
Rating:


Post a Comment