SPIKA KIFICHO AKEMEA WAWAKILISHI WANAOZUNGUMZIA MASUALA YA BUNGE MAALUM LA KATIKA NDANI YA BARAZA LA WAWAKILISHI
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho amekemea tabia ya
baadhi ya wajumbe kutofuata muongozo na kanuni za Baraza hilo kwa
kuzungumzia mambo ya siasa.
Amewataka
wajumbe kujadili mambo ya maendeleo ya nchi na kufanya kazi
waliyotumwa na wananchi na kuacha kujadili mambo ya siasa yanayoweza
kupelekea ubaguzi nchini.
Spika Kificho
ametoa maelezo hayo katika Ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi Chukwani kufuatia baadhi ya wajumbe kuzungumzia
masuala ya Muungano na Bunge la Katiba wakati kikao hicho kilipokuwa
katika kipindi cha masuala na majibu.
Amesema
kuzungumzia mambo ya Bunge la Katiba na Muungano wakati huu sio mahala
pake kwani inaweza kuleta ubaguzi na kutoweza kufikia lengo la kikao
hicho kinachoendelea kujadili mambo ya maendeleo.
“Sipendi
kusikia wazanzibari, sipendi kusikia watanzania wanafika pahala
kubaguana nasema haya kwa manufaa ya watanzania wote,” alikemea Spika
Kificho.
Amefahamisha
kuwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki wananchi na kuliweka pabaya
taifa kwani wao ni viongozi wanaotegemewa na jamii hivyo ni vyema
wakajenga heshima ili kutekeleza vyema majukumu yao.
Aidha
Spika Kificho amekataza masuala ya Bunge la Katiba na Muungano
yasijadiliwe wakati kikao hicho kinaendelea na mijadala ya Bajeti ya
Serikali kwa mwaka 2014/2015.
Wakichangia
kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2014/2015
mwakilishi wa Jimbo la Konde Suleiman Hemed Khamis amesema miradi ya
wananchi ni muhimu sana lakini miradi hiyo huwa haimaliziki kutekelezwa
na kufikia lengo lililokusudiwa.
“Miradi
huwa haimaliziki kutekelezwa kwa jamii kwani miradi hiyo inashindwa
kuwezeshwa na serikali na kutoweza kufika lengo lililokusudiwa mfano
mradi wa MECO wa barabara ya Wete Gando umeshindwa kumalizika kutokana
na kutolipwa pesa na bank kuwawezeshwa”, alifahamisha Mwakilishi huyo.
Mwakilishi
huyo amesema kuwa ili uchumi uweze kukuwa zaidi nchini, Serikali na
jamii zinapaswa kudhibiti vitendo vya uhalifu kwa watalii kwa kuondosha
vitendo vya wizi, uvamizi pamoja na wanasiasa kuacha kuzungumzia mambo
ya ugaidi.
Nae
Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani Hijja Hassan Hijja amesema biashara
nchini imekuwa ngumu kutokana na kuwepo kwa ushuru mkubwa unaosababisha
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa upande wa Zanzibar kushindwa
kufikia malengo ya kukusanya mapato iliyojiwekea.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
SPIKA KIFICHO AKEMEA WAWAKILISHI WANAOZUNGUMZIA MASUALA YA BUNGE MAALUM LA KATIKA NDANI YA BARAZA LA WAWAKILISHI
Reviewed by crispaseve
on
00:28
Rating:
Post a Comment