BREAKING NEWZZZ : MZEE SMALL AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 59
Habari za kusikitisha zilizotufikia hivi punde zinaarifu kuwa
Mwigizaji maarufu na mkongwe katika fani ya vichekesho nchini Tanzania,
Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small (59) amefariki dunia baada
ya kuugua kwa muda mrefu. Mzee Small amefikwa na umauti majira ya saa 4
za usiku wa Juni 7, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhumbili.
Akiongea kwa njia ya simu mke wa marehemu, Bi Fatuma Saidi,
aliithibitishia blog ya Father Kidevu , kuwa Msanii Said Ngamba hatunae.
Bi Said amesema kuwa marehemu mumewe amefikwa na umauti baada
ya hali yake kubadilika jana (Juni 7) asubuhi na kumbikiza Muhimbili
ambako alishinda nae akipatiwa matibabu na majira ya saa tatu usiku
alirudi nyumbani na kumwacha kijana wake akimwangalia mgonjwa na
ilipotimu saa tano usiku kijano huyo alirudi na kusema baba amefariki.
“Nikweli Mzee Small amefariki”….yalikuwa ni maneno machache
yaliyobenba uchungu mzito kufuatia kifo cha mumewe. Mipango ya Mazishi
inafanyika nyumbani kwa marehemu Tabata Mawenzi, Dar es Salaam.
Bamiza Blog inatoa salamu za pole kwa familia na wafiwa wote waliofikwa na msiba huyo.
BREAKING NEWZZZ : MZEE SMALL AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 59
Reviewed by crispaseve
on
23:56
Rating:
Post a Comment