Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hamisi Ramadhani Baba, maarufu kama ‘H.Baba‘
ameshindwa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu George Tyson
ulioagwa katika viwanja vya Leaders Club baada ya kupata homa kali
iliyompelekea aanguke ghafla wakati akijiandaa kuelekea msibani na
kukimbizwa hospitalini.
Mkali huyo mwenye vipaji lukuki ikiwemo uigizaji aliposti
picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa hospitalini na dripu
mkononi na kisha kuandika ”Naumwa sana nilikuwa najiandaa kwenye kumuaga mwenzetu #tyson nikaskia kizunguzungu nikaanguka apa nipo hosp”. Get Well Soon Bro
H.baba akiwa hospitalini na Dripu mkononi
H.BABA ASHINDWA KUMUAGA TYSON, ASHIKWA NA HOMA KALI
Reviewed by crispaseve
on
00:13
Rating: 5
Post a Comment